HOJA: KWA NINI TUNAWAJIBIKA KUOMBEA AMANI YA NCHI?

Askofu Sylvester Gamanywa
Mwangalizi Mkuu, WAPO Mission International.

©Verna Bowman
Nchi yetu iko kwenye mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu wa kuwapata Rais, wabunge na madiwani. Kama ambavyo tunaona vuguguvu la kampeni mwaka huu limekuja na uamsho mkubwa ambao nao una changamoto zake. Wakati huo huo, tayari kuna viashiria vinnavyotishia amani na utulivu kama hapatakuwepo na juhudi makini za kuzuia uvunjifu huo katika nchi. Ndipo siis kama kanisa tunaporejea kwenye maandiko matakatifu ili  kujikumbusha yanatwambia nini katika suala zima la kuombea amani ya nchi. Hata hivyo, msukumo wa kuombea amani ya nchi lazima ulenge muktadha wa maandiko ambayo tunapenda kuyanukuu kama mwongozo wa kuombea amani ya nchi.

Ufunuo mpya katika
kuombea amani ya nchi

“Lakini kabla ya mambo yote nataka dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili yatu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbebe za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yayo kweli.” (1 Tim.2:1-4)

Si mara ya kwanza kuwasilisha mada hii katika majukwaa mbali mbali ya kiibada na kimdahalo. Maandiko nliyoyanukuu kwa ajili ya mada hii, si mageni kabisa. Lakini ni muhimu nitoe sababu ni kwanini nimesukumwa kuleta hoja hii.

Sababu ya kwanza iliyonisukuma ni ufunuo mpya ambao nimeupata katika maandiko haya. Nasema ufunup mpya kwa sababu ipo tafsiri ya siku nyingi kuhusu matumizi ya maandiko haya. Tafsiri hii iliyozoeleka ni kufikiri kwamba maandiko haya yanawahamasisha “Waamini kuwaombea wafalme na wenye mamlaka wapate kuongoza nchi katika mazingira ya utulivu na amani.”
Hii ni tafsiri ya jumla.

Sasa ufunuo mpya ninaouwasilisha ni huu: “Maombezi kwa ajili ya wafalme na wenye mamlaka wataolinda uhuru wa kuabudu na kueneza injili katika mazingira ya utulivu na amani.” Tofauti iko wapi? Ipo kwenye kusudi la “kuombea amani” ni kwa ajili ya “kulinda uhuru wa kuabudu na kueneza Injili” Ufunuo huu unaungwa mkono na sehemu ya maandiko yasemayo:

“…..tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbebe za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yayo kweli…”

Ninachopenda kutilia mkazo tangu mwanzo mwa mada hii, ni kuhusu Mukhtadha wa maandiko ya kuombea amani ya nchi, yamelenga utekelezaji wa agizo kuu la Mungu kumleta Yesu duniani. Mungu anataka tuishi maisha ya utauwa na ustahivu; na pili, Mungu anataka jamii ya watu wasioamini wafikiwe na Injili na kuokolewa, na kufundishwa kusimama katika imani sahihi, na mambo haya yawafikie walengwa kwenye mazingira ya utulivu na amani.

Sababu ya kuombea
wafalme na wenye mamlaka

Baada ya kufafanua kile nilichokiita ufunuo mpya nilioupata kutoka kwenye maandiko ya kuombea amani ya nchi, naomba sasa nijikite kwenye sababu za msingi za kuombea “wafalme na wenye mamlaka”. Ninapenda kutoa tahadhara ya kuamcha kuomba kwa mazoea ya kidini na turejee kwenye muktadha wa maandiko.

Kuwaombea wafalme na wenye mamlaka katika eneo la hekima katika kupanga na kufanya maamuzi kwa ajili ya raia wanaowaongoza. Mtume Paulo ambaye aliteuliwa kuwa Mtume wa mataifa na wafalme alikuwa na ufunuo juu ya maisha ya wafalme na wenye mamlaka katika enzi zake. Aliwaona jinsi walivyozungukwa na washauri ambao ni mawakala wa shetani maarufu kama waganga wa tunguli na wanajimu. Hawa ndio waliokuwa na ushawishi kwa wafalme kwa sababu ya ujanja na ufundi wao katika mambo ya ushirikina na uchawi.

Mara kadhaa Paulo aliwahi kumkemea mchawi mmoja aliyekuwa mshauri wa kiongozi wa dola ya kirumii ambaye alivutiwa na Injili ya Paulo, lakini yule mganga na mchawi akajaribu kumzuia asisikilize Injili na ndipo Paulo akamkemea na kumfanya kuwa kipofu kwa muda.

Ni kutokana na uzoefu huu Paulo alimwagiza Timotheo asimamie mkakati wa kuwaombea wafalme na wenye mamlaka ili wapokee hekima ya Mungu itakayosaidia kutambua uwepo wa watumishi wa Injili ambao wana wajibu wa kuhubiri Injili ya wokovu na hivyo watoe uhuru wa kuabudu na watu wote wapate kuokolewa na kujya yaliyo kweli.

Tatizo kubwa linanlotukabili hapa kwetu na nchi nyingi za kiafrika ni kwamba tunataka “kuwepo kwa amani ya maslahi ya kiuchumi na kijamii” lakini pasipo watu kuhubiriwa injili ya kweli ya ukombozi wa Yesu. Pamoja na nchi kuendelea kuporomoka kimaadili na kuzama kwenye uchafu wa kitabia na uasi wa kutisha kiimani bado tunataka tuendelee kuishi kwa utulivu na amani kwenye mazingira yaliyoharibika kimaadili.

Na sio kwamba napinga suala la kuombea amani na utulivu wa kisiasa na kiuchumi kwa ajili ya watu wote. Ninachosisitiza ni kwamba sababu makini za kuombea wafalme na wenye mamlaka ni amani na utulivu vihamasishe uhuru wa kuabudu na kueneza injili ya ukombozi wa Yesu Kristo kwa watu wote. Kwa sababu kama ilivyoandikwa kwamba “….Hili ni zuri, nalo lakubalika mbebe za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yayo kweli…”


Katika A/K kuliwepo na aina 4 za uvumba:

“BWANA akamwambia Musa, jitwalie manukato mazuri, yaani natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na view kipimo kimoja; nawe utaufanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenezaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu, na baadhi yake utakayoponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokuwa nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.” (Kut.30:34-36)

Natafi
Shekelethi
Kelbena
Ubani

Uvumbi uliofukizwa hemani ulitenegezwa kwa viungo maalum na haikuruhusiwa uvumba wa aina hiyo kutenegenezwa kwa matumizi mengineyo isipokuwa hemani/hekaluni peke yake

Mtume Paulo, alipokea ufunuo wa Roho Mtakatifu, kwamba, maombi ambayo kanisa linatakiwa kuombea nchi lazima yazingatie viwango vya manukato ya uvumba ambayo tafsiri yake ndiyo hayo mambe 4                                 

Dua      -           Mlango wa dharura, kumsihi Mungu aingilie kati kuokoa jahazi, kunusuru janga
Sala      -           Upatikanaji wa mahitaji binafsi na ya lazima
Maombezi         Kuwasilisha shida za mtu mwingine mbele za Mungu kwa mzigo ule ule kama wako
Shukrani          Kuwasilisha mrejesho kwa Mung kwa mambo aliyotenda


Uwezeshaji wa utekelezaji
wa mpango wa Mungu

Wajibu wa kudumu                  =          Kila siku, kila mwezi, kila mwaka?
                                                            Kipaumbele kwa kila aina ya maombi


TAFSIRI YA MISAMIATI


Msomaji mpenzi

Kuanzia Jumapili hii, pale BCIC Mbezi Beach, kwenye ibada kuu ya huduma za Roho Mtakatifu tutaanza na kuombea nchi katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi, siku ya uchaguzi wenyewe, siku ya kutangaza matokeo, mpaka siku ya kuapishwa Rais mpya.

Kipaumbele ni kudumisha utulivu na amani kwa ajili yetu kwa sababu viko viashira vya waziwazi vinavyotishia kuvunjika kwa amani.

Ikiwa kanisa tutatoa kipaumbele kabla ya mambo yote tukafanya dua, sala, maombezi na shukrani, tuna imani tutavuka salama hata kama Shetani alikusudia mabaya, lakini UVUMBA WA MANUKATO TUTAKAOWASILISHA MBELE ZA MUNGU utaokoa na kulinusuru taifa letu.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.