KUDHARAU NDOTO YA MTU SIO TIKETI YA NDOTO YAKO KUFANIKIWA

Picha ya Rais wa Marekani Barack Obama enzi hizo kabla ndoto haijatimia akiwa Kenya ©naij
Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.


KUDHARAU NDOTO YA MTU SIO TIKETI YA NDOTO YAKO KUFANIKIWA. Maisha bila kuwa na ndoto ni kuishi maisha ya uangamivu na upotevu.Maisha yeyote yasiokuwa na kusudi na lengo huwa hayana maana na furaha haimo ndani yake.Pasipo kusudi na malengo kwenye maisha mtu haamua kuishi vile atakavyo na kufanya kile atakacho bila kujua anajiletea uangamivu wake mwenyewe.Maisha ni zawadi ambayo kila mmoja amepewa kwa wakati wake,Maisha ni Zawadi ambayo ndani yake kuna rasilimali za kila namna.Mtoa Uhai aliwekeza kila rasilimali muhimu ndani ya aliyepewa uhai atakayoihitaji kwenye kipindi cha kuishi kwake.Utambuzi na Ugunduzi wa rasilimali hizo hutegemea maamuzi ya aliyepewa na sio aliyetoa rasilimali hizo. Hakuna mtu anayeweza kuitimiza ndoto yake akiwa pekee yake kila mmoja ana muhitaji mwingine ili kuweza kutimiza ndoto yake.Watu ambao tunakutana nao kila siku na kuishi nao wana mchango mkubwa kwenye maisha yetu katika kulielekea kusudi na lengo la maisha yetu.Ndoto tulizo nazo muda mwingine zinategemea namna tutakavyo watumikia wengine,Unaweza kukuta katika kumtumikia mwingine na ndipo pia ndoto yako inapotimia . Moja ya Rasilimali kubwa kwenye maisha yetu ya kila siku ni Watu Wanaotuzunguka katika maeneo mbali mbali iwe kazini,nyumbani,kanisani,msikitini na hata kwenye shughuli mbali mbali za kijamii.Hakuna mtu ambaye anaweza kuishi pekee yake na kujitosheleza kwa kila jambo kila mmoja ana muhitaji mwingine ili kuweza kufikia mambo fulani kwenye maisha yake.Ni Muhimu sana kujifunza namna ya kuhusiana na wengine kwa ukaribu na utaratibu mzuri maana hao ndio sehemu ya kuelekea ndoto yako.Ukifwatilia watu wengi waliofanikiwa utagundua wamejiwekea mfumo mzuri wa kuwa na mahusiani mema na wengine kwenye Nyanja mbali mbali walizopitia maishani mwao bila kujali uwezo wa watu ambao walikutana nao maishani mwao.Muda mwingine unaweza usione sababu ya kuwa na mahusiano mazuri na wengine kwa sababu hauko kwenye kipindi cha uhitaji wa aina fulani ,kuna wakati utakapokuwa na uhitaji utagundua kuna watu ulikutana nao kwenye maisha na wangewezakuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto yako unayopita lakini kwa sababu haukuona umuhimu wa kuwa na mahusiano mema nao inakulazimu kutumia gharama kubwa pasipo sababu ya msingi wakati mahusiano yako mazuri na wengine yangeshatatua changamaoto yako kwa urahis zaidi. Hauwezi kufanikiwa zaidi ya mahusiano uliyojitengenezea na watu wengine wanaokuzunguka.Tunahitaji watu kufikia ndoto zetu , Watu wengine hutumia gharama kubwa kuwalipa watu fedha ili kupata nguvu kazi ya mwanadamu ambayo mashine haziwezi kuzifanya .Unapojitengenezea mahusiano mabovu na wengine tarajia kutofika kiwango cha juu cha ndoto yako. Ubora wa Ndoto sio kufikia kilele cha Mafanikio tu bali ni mchakato mzima mpaka kufikia kiwango hicho cha mafanikio.Unaweza ukawa umefikia mafanikio ya ndoto uliyoyahitaji lakini umeacha makovu na vilio kwenye mioyo ya watu wengine ,jambo kama hili litakupa furaha na muda na sio ya kudumu baada ya muda mfupi utaanza kushuhudia poromoko la kasi sana kwenye mafanikio uliyoyafikia kwa wakati huo.Ni muhimu kuhakikisha unajenga mahusiano bora na wengine kwa gharama yeyote maana watu ni ni rasimali kubwa zaidi na utakapowapoteza watu ni ngumu kuwarejesha tena katika kiwango kile kile cha mahusiano kilichokuwepo mwanzo .Jenga tabia njema ya kuwaheshimu na kuwathamini wengine pia. Watu Wanaweza Kukupandisha Juu na Wanaweza Kukushusha Chini.Ni muhimu kutambua mchango wa wengine kuelekea kwenye ndoto zako,si kila mtu anakiwango kilekile sawasawa na ndoto zako ,wakati mwingine ndoto za wengine zinaweza kuonekana ni dhaifu kuliko zako lakini katika udhaifu huo pia wewe utahitaji aina fulani ya mchango wake kwenye kufikia ndoto zako. Kuna wakati wengine wanaweza kujitoa kwa hali na mali ,kujitoa kwao kwako ndio inaweza ikawa ni sehemu ya ndoto zao kwenye maisha yao. Kuna watu wengine hupenda kuwatumikia wengine bila kujali aina ya malipo watakayoyapata kwa wakati husika lakini ili hali ule utumishi wao kwako unawapa furaha ya kweli na ya ndani kwenye mioyo yao. Kumbuka utumishi wao kwako ndio unaokuongezea thamani ya wewe kuweza kufikia ndoto zako katika kiwango cha juu.Usidharau mchango wa kila mmoja maana watu hao hao watakapoacha kutoa utumishi wao kwako ndipo pengo la utumishi wao kwako utaanza kuliona na utakuwa umeshachelewa na ndipo hasara kubwa inaweza kutokea. Mwisho Unaweza kununua bidhaa lakini hauwezi kununua mahusiano bora na watu wengine. Mahusiano bora na wengine ni jambo ambalo linatengenezwa na ni mchakato wa muda mrefu ,Mahusiano bora na wengine sio tukio bali ni safari ya kitambo ambayo inahitajika kujitoa kwa wengine bila kujali aina ya faida unayweza kuipata kwa wakati husika.Ni muhimu kujenga tabia ya kuheshimu na kushiriki kwenye ujenzi wa ndoto za watu wengine ili kuweza kupata nafasi njema ya wewe kujenga ndoto yako katika mazingira mazuri na yasiokuwa na tashwishwi zisizokuwa na msingi wowote.Ni Muhimu kuhakikisha unajifunza mbinu mbali mbali za kuboresha na kujenga mahusiano mema na mazuri na watu wengine. E-mail: naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless You All.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.