KWA TAARIFA YAKO: HII NDIO ALBUM AMBAYO HAIKUWASUMBUA JOYOUS CELEBRATION KUREKODI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. KaribuKWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kwa kundi ambalo mwaka huu litakuwa likirekodi DVD yake ya 20 toka kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 20 iliyopita huko Durban nchini Afrika ya kusini. Nazungumzia Joyous Celebration ambayo ni chimbuko la waimbaji wengi maarufu wa nchini humo ambao kwasasa wanamafanikio ya kimuziki toka wapate mafunzo kisha kujitoa kundini na kujitegemea.

KWA TAARIFA YAKO Joyous inarekodi matoleo mapya kila mwaka mwezi December ingawa toleo moja la 13 ilibidi warekodi mwezi February kutokana na mambo kuingiliana. Moja ya kazi ngumu ambayo waimbaji hao huifanya ni kuandaa tukio zima la kurekodi kisha kurekodi toleo husika lakini pia mara baada ya kumaliza kurekodi, kundi hilo uenda studio ili kujazia sauti na muziki kwenye toleo walilolirekodi ili kulifanya kusikika vizuri sana katika kiwango bora kazi ambayo huwa ni ngumu hasa pale ambapo mwimbaji au waimbaji wanapoimba vibaya wakati wa tukio halisi kwani inakuwa vigumu kurekebisha makosa hayo wawapo studio.KWA TAARIFA YAKO moja kati ya album ambayo kundi hilo pamoja na waimbaji wake wanajisifu kwayo kwamba haikuwapa kazi ngumu katika kurekodi na hata hawakutakiwa kufanya KWA TAARIFA YAKO kwa mujibu wa moja wa aliyekuwa nyota wa sauti ya pili wa kundi hilo ambaye kwasasa amemaliza mkataba Duduzile Tsobane ameiambia GK kwamba, kurekodi kunakuwaga na kazi ngumu sana mpaka DVD na CD kutoka, kwakuwa baada ya kurekodi hufanya kazi ya ziada studio kupendezesha toleo husika kisha kulitoa
Ambwene akiwa na Duduzile
kazi ngumu studio kutokana na kutokuwa na makosa makubwa basi ni album ya 15 part 1 na part 2 ambazo ni moja kati ya kazi bora kuuzwa na kundi hilo hata waimbaji wenyewe wakiipigia chapuo album hiyo.

KWA TAARIFA YAKO Dudu amesema katika matoleo yote toka ajiunge Joyous toleo ambalo waimbaji aliotumika nao kwa wakati huo pamoja na viongozi wa kundi ni toleo la 15 halikuwapa shida kabisa kwakuwa live recording ilikwenda vizuri sana, sauti na vyombo vilisikika vizuri sana kwahiyo hawakuwa na haja ya kujazia sana kuipendezesha kwakuwa tayari ilikuwa imejitosheleza toka siku ya tukio. KWA TAARIFA YAKO aidha mwimbaji huyo amesema mara nyingi kundi linapopokea waimbaji na wapigaji wapya huku wa zamani wakiondoka, mara nyingi toleo linalofuata huwa linapiogiwa kelele kwamba haliko kwenye mstari kitu ambacho amesema hutokana na timu mpya bado kuzoea mkong'osio wa kundi hilo, mfano amesema Joyous 11 haikupokelewa vizuri kama walivyotarajia lakini Joyous 12 kundi lilisimama katika ubora wake na kutoa toleo hilo ambalo amesema ni moja kati ya kazi bora za Joyous.Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.