KWA TAARIFA YAKO: HII NDIO ORODHA YA WACHUNGAJI MATAJIRI ZAIDI DUNIANI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Askofu David Oyedepo
KWA TAARIFA YAKO hii leo tunakutajia 10 bora ya wachungaji matajiri duniani, ambao wamekuwa wakitajwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na huduma zao sambamba na waumini wanaoabudu katika makanisa hayo. Kwa mujibu wa moja ya mtandao maarufu wa Full Networth katika orodha hiyo wachungaji wanne kutoka Nigeria ni miongoni mwa wachungaji waliomo katika orodha hiyo. KWA TAARIFA YAKO Full networth umedai askofu maarufu kutoka Nigeria mwenye waumini zaidi ya milioni duniani,  David Oyedepo ndiye anashikilia nafasi ya kwanza kwakuwa na utajiri unaokaribia dola za kimarekani milioni 150. Mchungaji Oyedepo anachunga huduma yake ijulikanayo kama the Living Faith World Outreach Ministry aliyoianzisha rasmi mwaka 1981 huku ibada yake ikihudhuriwa na watu takribani 50,000 kila jumapili.

Mchungaji Chris
KWA TAARIFA YAKO mtandao huo umemtaja mchungaji Chris Oyakhilome (pastor Chris) kushika nafasi ya pili akiwa na utajiri unaokisiwa wa dola milioni 50. Mchungaji Chris ni kiongozi wa huduma ya Christ Embassy Church lenye waumini sehemu mbalimbali duniani, huku ikidaiwa kwamba watu 40,000 huhudhuria ibada kila jumapili kanisani kwake. Mchungaji Chris pia ni mfanyabiashara akiwa amewekeza kwenye mambo ya hoteli, media huku mahubiri yake yakidaiwa kuwalenga wajasiriamali na wanasiasa ili waweze kufanikiwa kwenye shughuli zao.

Mchungaji Benny Hinn
KWA TAARIFA YAKO Mchungaji maarufu wa Marekani Benny Hinn ametajwa kushika nafasi ya tatu kwa mujibu wa mtandao huo, akiwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 42. Mhubiri huyu mwenye asili ya Israel na Marekani anasifika kwa mikutano yenye miujiza lakini pia ni mwandishi mzuri wa vitabu. Aidha mtandao huo umemtaja mchungaji Creflo Dollar wa Marekani anayesimamia huduma ya World changers Church International huko Marekani anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 27, pia ikumbukwe mchungaji huyu alivipamba vichwa vya habari nchini Marekani mwaka jana alipowataka waumini wake wamchangie pesa ili anunue ndege yake binafsi ya kifahari, jambo lililopingwa sana na watumishi wengine akiwemo mwimbaji maarufu Krik Franklin.

Creflo Dollar
KWA TAARIFA YAKO Mtandao huo umemtaja mhubiri na mwinjilisti mkongwe na maarufu duniani Billy Graham  ambaye amesifika kwa mikutano yake mikubwa ya injili ndani na nje ya Marekani huku watu wakiponywa na kutajwa kama baba wa wahubiri duniani, kwamba ameshika nafasi ya tano akiwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 25. Kwa upande mwingine nafasi ya sita imeshikwa na mchungaji maarufu wa Marekani askofu TD Jakes wa kanisa la the Potters house lenye waumini zaidi ya 30,000 nchini humo, kwamba anautajiri wa dola za kimarekani milioni 18 huku nafasi ya saba ikichukuliwa na mtume TB Joshua wa Nigeria akiwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 15.

Askofu TD Jakes
KWA TAARIFA YAKO Nafasi ya saba imeshikwa na mchungaji Mnigeria anayevuma sana nchini Uingereza ambako ndiko alikoweka makazi yake mchungaji Matthew Ashimolowo anayechunga huduma ya Kingsway International Christian Centre (KICC) anatajwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 10, huku mchungaji mwenzake kutoka Nigeria Chris Okotie ambaye pia ni mwimbaji akichunga huduma ya the Household of God Church International Ministries yeye anautajiri wa dola za kimarekani milioni 10 akiwa ameshikilia nafasi ya 9.

Mchungaji Matthew Ashimolowo
KWA TAARIFA YAKO mchungaji aliyetajwa kushika nafasi ya 10 ni Joseph Prince wa Singapore mwenye utajiri wa dola za kimarekani milioni 5 akiwa anachunga kanisa la New Creation lililopo nchini Singapore likitajwa kuwa moja kati ya makanisa makubwa kwa bara la Asia. Mchungaji huyu anatajwa kulipwa mshahara wa dola za kimarekani 550,000 kwa mwaka huku taarifa za fedha katika kanisa lake kwa mwaka linapokea bili ya dola za kimarekani milioni 50.

TB Joshua

Chris Okotie

Mwinjilisti Billy Graham 
Joseph Prince wa Singapore
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.