KWA TAARIFA YAKO: MKASA WA MWIMBAJI NYOTA KUKOSA KODI YA NYUMBA HUKU MKEWE MJAMZITO

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. KaribuKWA TAARIFA YAKO hapana shaka utakubaliana nami kwamba moja kati ya makundi yaliyofanya vyema na kuuweka mziki wa injili nchini kuwa juu, kundi la Kijitonyama Upendo Group ni moja wapo, kwa jinsi hali ilivyokuwa ukikutana na kundi hilo enzi hizo, kitu kimojawapo kitakachokujia akilini ni kwamba, waimbaji wa kundi hilo walikuwa na pesa ama kwa namna nyingine maisha yao yalikuwa safi, hasa ukizingatia kanda walizokuwa wakiuza watembeleapo sharika mbalimbali. Lakini hiki kilichonenwa na mmoja wa waliokuwa nguzo na mwalimu wa kundi hilo bwana Joshua Mlelwa utabaki ukisikitika.

KWA TAARIFA YAKO kuvuma kwa Upendo Group kulitokana na juhudi kubwa za waimbaji lakini Joshua Mlelwa kama mwalimu na mwanzilishaji wa nyimbo za kundi hilo alikuwa ni kitambulisho tosha popote kundi hilo lilipokwenda kuhudumu, lakini cha ajabu ambacho amekuja kuweka wazi hivi karibuni akihojiwa na Uncle Jimmy Temu kupitia blog yake, amesema licha ya umaarufu aliokuwa nao na kuhudumu katika kundi la Upendo Group, lakini hakuwa na pesa za kutosha kuendesha familia yake, ilifikia mpaka wakati ambao mkewe aitwaye Lilian ambaye pia alikuwa mwimbaji wa kundi hilo, akiwa mjamzito wa kupata mtoto wao wa pili, walitakiwa kuhama kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi kwasababu walikosa kodi na kuhamia Bunju kwenye kibanda ambacho Joshua alipewa kujihifadhi kwa muda wakati anaweka mambo yake sawa.

Joshua Mlelwa akiliongoza kundi la KUG enzi hizo, mkewe akiwa wa kwanza kushoto


KWA TAARIFA YAKO ikumbukwe waimbaji wa kundi la Upendo Group walikuwa hawana kazi nyingine ukiacha uimbaji, hali iliyofanya waweke juhudi zaidi kwenye huduma ambayo hata hivyo haikuweza kuwasaidia hasa katika suala la kimwili yaani kipesa zaidi ya kuweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. KWA TAARIFA YAKO ikumbukwe kwamba kundi hilo kwasasa haijulikani kama bado lipo au lilishakufa kutokana na waimbaji wake kuendelea na shughuli zao binafsi na wengine kuanza kurejea kwenye kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambako ndiko waimbaji waliokuwa wakiunda kundi hilo walikotokea.

KWA TAARIFA YAKO ukiachana na habari hiyo Joshua pia aliweka wazi namna alivyompata mkewe Lilian ambaye alikuwa mmoja kati ya waimbaji nyota wa kutegemewa wa Uinjilisti Kijitonyama, ambapo Joshua aliweka wazi kwamba licha ya mkewe kufuatwa na watu mbalimbali wenye nyadhifa za heshima katika jamii wakiwemo watu wanaofanya kazi bank, lakini Lilian aliwakatalia hao wote na kumkubali Joshua ambaye kwa wakati huo ndio kwanza alikuwa amekuja mjini akitokea mkoani. Nyota zao zilianza kuchanua baada ya kuimba wimbo wa kilio Tanzania wakiwa na Uinjilisti Kijitonyama.


     PATA MOJA YA NYIMBO ZA UPENDO GROUP KUTOKA TOLEO LA KWANZA

Katika yote, ukimtumikia Mungu kwa uaminifu wala hatokuangusha. Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.