MAMBO MACHACHE UNAYOWEZA KUYAFANYA KUBORESHA MAMBO MBALI MBALI MAISHANI MWAKO


Na Faraja Naftal Mndeme, 
GK Contributor.
MAMBO MACHACHE UNAYOWEZA KUYAFANYA KUBORESHA MAMBO MBALI MBALI MAISHANI MWAKO.

MATUMIZI YA MUDA.
Muda ni rasilimali ambayo ikipotea imepotea,Muda ni mchache na mambo ya muhimu ni mengi.Unapohitaji maboresho kwenye jambo lolote kwenye maisha yako,jambo la kwanza imekupasa kufwatilia namna unavyotumia muda wako kwenye maswala mbali mbali kila siku.Hakikisha unachunguz kwa ukaribu kila dakika na kila sekunde unavyoitumia maishani mwako, je unaitumia kwa faida au kwa hasara?Unapofahamu namna unavyotumia muda wako kwanza inakurahishia kujua hatua inayofwata kwenye maisha yako.Hauwezi kuboresha maisha yako kila siku iwapo haujui namna unavyotumia muda wako. Mfano Mzuri Unaweza Kukuta Unajribu kutmia muda wa Nusu Saa Kuandika Barua Ya Maelezo kwa Mtu Kumbe Ungempigia simu ungetumia dakika tano na mngeongea na kuelewana .Ni Muhimu unahakikisha unaokoa muda kila inavyowezekana kwenye mambo yasiyokuwa na Ulazima.

TAMBUA UDHAIFU
Kabla ya kuamua kuboresha maisha yako hakikisha unatambua udhaifu ulio nao ili kuweza kuudhibiti.Ni ngumu kuweza kuendelea mbele iwapo hautaweza kuujua aina ya udhaifu wako ambao mara nyingi huwa chanzo cha makosa mengi maishani mwako.Udhaifu Wako ndio unaoweza kukurudisha nyuma.Mara nyingi tunaposhindwa jambo huwa tunaangalia tulipoangukia badala ya kuangalia tulipojikwaa.Ni muhimu kuhakisha udhaifu ulio nao hauwi kikwazo kwenye kuleta matokeo bora unayoyatarajia kila siku.Ni Muhimu kulitambua tatizo ili kuweza kupata tiba ya tatizo hilo lisiweze kujirudia tena na kukufanya kurudi pale pale kila siku.Usipotambua udhaifu ulio nao utajikuta kila siku unarudi pale pale na hautaona hatua mpya kwenye maisha yako.

MTAZAMO CHANYA
Maisha yetu namna yalivyo kila siku yanatulazimisha kuwa na mtazamo hasi badala ya chanya kwenye maisha yetu.Ni rahisi kufikiria kushindwa kuliko kufikifiria kushinda.Mtazamo chanya kwenye kila jambo unalolifanya kila siku ni jambo linalohitaji kupaliliwa na kuboreshwa kila siku .Mtazamo Chanya si jambo ambalo linaibuka tu kama Uyoga bali ni Mbegu Inayopandwa Maishani Mwa Mtu na Kuendelea Kutunzwa na Kulindwa kwa gharama zote maana utakaposhindwa kufanya namna hivyo ni kuruhusu anguko lako mwenyewe kila siku.Kwa Asili Maisha Ya Mwanadamu Yalivyo Hukufanya Ujijenge Mtazamo hasi kwenye Kila Jambo,Gharama ya Kujenga Mtazamo Chanya Ni Kubwa lakini Gharama ya Kuwa na Mtazamo Hasi ni Kubwa Zaidi.

USAWA WA MAMBO
Kila jambo la kwenye maisha lina kiasi linapozidi linakuwa kero.Unapoamua kujenga na kuboresha maisha yako kila siku ni muhimu kuhakisha unakuwa na usawa wa vitu kwenye kila Nyanja , Usiwekeze eneo moja zaidi na ukasahau lingine maana unaweza kujikuta unajenga upande mmoja na unabomoa upande mwingine jambo ambalo litakufanya utumie muda mwingi pasipo na ulazima.Fikiria iwapo una familia halafu Muda Mwingi Uwe Unatumia Kazini bila Kuwa na Muda wa Familia kwa Kisingizio unatafuta fedha.Kiukweli fedha utaipata lakini ukirudi kwenye familia yako utakuwa kama mtu mgeni maana haukuwa sehemu ya familia .Itakulazimu uunze gharama nyingine mpya ya kuanza kuijijenga kwenye familia tena.Ni muhimu kuwa na kiasi na usawa wa mambo kwenye maisha katika kila unachokifanya.

FANYA UTAFITI WA KINA.
Mara nyingi maamuzi ya maisha ya watu wengi yamejengwa kwenye mihemko badala ya utafiti wa kina wenye hoja za msingi na ushawishi wa maana ambapo hata maamuzi ya kuboresha jambo yatakapokuwa yamefanyika matokeo ya msingi na malengo yanaweza kufikiwa na gharama ikiwa inajulikana tangu mwanzo wa safari.Maamuzi mengi yanayofanywa chini ya mihemko huwa na muda mchache na matokeo yake huwa sio ya kudumu na yenye kuleta tija kwa kipindi kirefu.Ni muhimu kufanya utafiti wa kina kabla ya jambo hujaliamulia kulifanya maamuzi ili kuweza kufikiwa na kapata matokeo halisi na bora yaliotarajiwa tangu mwanzo wa safari.
E-mail: naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless You All

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.