MKUU WA WILAYA AZINDUA VITABU VYA MWALIMU LILIAN NDEGI

Jumapili ilikuwa siku njema kwa wakazi wa Dar waliofika Kanisa la Living Water Center,Kawe. Ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu (MJUE MWANAMKE, USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA) vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa kanisa hilo.

 Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama wenyeji Living Waters, Upendo Nkone, GUG Dancers na More Than Enough Band.

Katika uzinduzi wa vitabu hivyo Mkuu wa Wilaya pia aliendesha zoezi zima la kuviuza, ambapo kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.

Ukataji wa ulikuwa sehemu ya tukio ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kufanikisha uandishi wake wa vitabu.

Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.
Apostle Onesmo Ndegi, kiongozi wa Kanisa la Living Water Center ambaye pia ni mume wa mwandishi wa vitabu, Mwl Lilian Ndegi. Amejivunia mkuu huyo wa wilaya na kusema kwamba ni kijana wake na anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kuongeza kwamba amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu, hivyo Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa kiongozi wa wilaya hakukosea.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda alipokuwa akizungumza baada ya kuzindua vitabu 

Mh.Paul Makonda akizindua vitabu 
Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana
Mh. Paul Makonda akilishwa keki Mwl Lilian Ndegi mwandishi wa vitabu vilivyozinduliwa
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa, Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua

Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo
Mchungaji Deborah Ntepa kutoka Oasis Healing Ministry alikuwepo katika uzinduzi huo
Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda

Mwl Lilian Ndegi na Upendo Nkone wakicheza mbele za Bwana ilikuwa full shangwe
Mh. Paul Makonda wa kushoto, katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center pamoja na mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi.
Mh.Paul Makonda na Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya mabinti  wa kanisani hapo.
Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa  kanisani hapo.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.