PROMOTA ASABABISHA KUNDI MAARUFU LA INJILI AFRIKA YA KUSINI KUIMBA CHINI YA KIWANGO

Baadhi ya waimbaji wa Worship House waliorekodi toleo la 12

Kundi maarufu la muziki wa injili nchini Afrika ya kusini la Worship House lenye makazi yake Limpopo nchini humo limejikuta katika wakati mgumu siku ya jumamosi iliyopita baada ya onyesho lao la kuzindua DVD mpya ya 12 kwenda chini ya kiwango na kuibua minong'ono kwa wahudhuriaji.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa kundi hilo lililochini ya askofu Isaac Dagada wa Christ Worship House, zinadai kwamba onyesho la uzinduzi huo lilikuwa limeuzwa kwa promota ambaye hakuwekwa wazi na kwamba waimbaji hao walishindwa kukata kiu ya wahudhuriaji baada ya vyombo vilivyotumika kuwa chini ya kiwango na kusababisha watu kudai kurudishiwa pesa zao.

Kutokana na hasira zilizoonyeshwa na wahudhuriaji hao kupitia jumbe walizotuma kwenye ukurasa wa ndani wa kundi hilo kwenye Facebook kumemfanya mmoja wa viongozi wa kundi hilo na mtoto wa askofu Dagada aitwaye Patience kuwaomba radhi watu wote kwa kilichotokea na kwamba kundi hilo linapanga kurudia tena onyesho hilo la uzinduzi ambalo litafanyika bila kiingilio ikiwa njia moja wapo ya kutuliza hasira za mashabiki wao.

Kundi la Worship House limejizoelea mashabiki ndani na nje ya Afrika ya kusini kutokana na aina ya nyimbo za kitamaduni wanazoimba kupitia matoleo wanayorekodi kila mwaka. Ambapo tangu kuanza kwake tayari limejinyakulia tuzo mbalimbali pamoja na kutajwa kwenye vipengele vya kuwania tuzo za SAMA.Tazama moja ya kazi za Worship House project 7Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.