SOMO: KUTII NA KUNYENYEKEA - KING SAMKUTII NA KUNYENYEKEA
Isaya Isaiah 1:19
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

Unaweza kutii kumeza dawa alizokuandikia dakitari ili usife lakini uwezi kutii andiko alilosema Yesu kwa kupigwa kwa Yesu sisi Tumeponywa,
Unaweza kutii kuchelewa kutoka kwenye sherehe au arusi kwa sababu wamechelewesha mandalizi,lakini uwezi kutii kusubiri kuchelewa kwa ibada kwa sababu Mchungaji amezidisha muda kidogo,
Unaweza kutii masaa ya kwenda kulipa madeni lakini uwezi kutii masaa ya kwenda kuomba mbele za Mungu sasa unatakaje Mungu akujibu mambo yako wakati wewe si mtiifu?
Uwezi kuchelewa safari yako unakokwenda Kama ni kwa gari au kwa Ndege,Bali unaweza kuchelewa kwenda kanisani,

Unaweza kuwa mwaminifu kwa Bosi wako,lakini kwa Mungu wewe siyo mwaminifu,
Unaweza kutii mme wako au mke wako lakini uwezi kumtii Mungu,
Unaweza kutii Sheria za barabarani lakini uwezi kutii sheria za Mungu,

Unaweza kutii kula kila kitu atakachokuambia dakitari lakini si raisi kula Mungu alichosema,
Yohane John 6:49
Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa.
50 Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.
51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Kama vile unavyotii sheria za duniani kujiepusha na adhabu ndivyo ilivyo usipotii sheria za Mungu unajipatia adhabu,bora adhabu ya mwanadamu au ya Mungu
2 Samueli 2 Samuel 24:14
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.

Anavyoweza kukutendea mwanadamu kwa kutokutii kwako,Mungu ni zaidi Kaa ukijuwa ilo kwanzia leo ili ubadilike katika jina la Yesu,
Waroma Romans 13:4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
5 Kwa hiyo ni lazima kutii, si kwa sababu ya ile ghadhabu tu, ila na kwa sababu ya dhamiri.

Unaweza kupoteza kila kitu katika maisha yako hata Kama uliombewa ukapokea kutoka kwa Mungu Kama ukikataa kumtii Mungu yeye anaweza kukushusha japo ni yeye aliyekupandisha na kukuweka hapo ulipo badilika katika jina la Yesu,
1 Samueli 1 Samuel 15:22
Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Kama Abraham hakutii kuondoka wakati Mungu amemuambia atoke katika nchi ya jamaa zake na baba yake,leo Israel wasingekuwepo,pili Sarah angebaki tasa,Kama wewe ulipokataa kutii kuna biashara ambazo hauna ulitakiwa ziwepo pili upo jinsi ulivyo kwa sababu ya kutokutii kwako usingekuwa hivyo,pili haujafanyika vile Mungu alitaka uwe kwa sababu haumtii Mungu,
Mwanzo Genesis 12:1
BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

Je unataka mema mtii Mungu tii Neno lake nawe utakula Mema kutoka kwake katika jina la Yesu UBARIKIWE na Yesu Kristo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.