SOMO: NAMNA YAKUMLEA MTOTO KATIKA NJIA IMPASAYO (7)

Kelvin Kitaso,
GK Contributor.

Mara ya mwisho tulianza kutazama nafasi ya familia katika melzi bora ya mtoto. Bofya hapa ili kusoma kabla ya kuendelea na leo.

Haukuizalia jehanamu watoto

Dada yangu (Ester) alinieleza kwa kumaanisha sana maneno haya akisema, “mimi sitozaa watoto kwa ajili ya Jehanamu” kwa maana ya kuzaa watoto ambao wataishia kwenda katika ziwa liwakalo moto.
Ni wazi sana kuwa BWANA wetu Yesu alikuzwa kwa kuwa na ibada hizi za nyumbani na ndiyo maana aliwauliza sana waalimu wa sheria maswali ambayo ilisababisha wamshangae kwa ile hekima ila ni matokeo ya kujifunza nyumbani.
Wafunze watoto wako kuwa na tabia ya kusoma neno na vitabu mbalimbali ili wakue katika hekima, ila itakuwa ina nguvu kubwa zaidi kama wewe binafsi ni msomaji.
Ibada za pamoja uwa pale baba na mama wanapopanga muda pamoja na watoto wa kukaa pamoja, kusoma na kuchambua neno pamoja na kusifu pamoja na kuomba pamoja. Na ibada hizi uambatana na maswali mbalimbali ili kukuza uelewa wa wanafamilia katika neno.

Lengo la ibada hizi uwa katika kuwakuza watoto katika njia iwapasayo ambayo itawasaidia kuendelea kuwa karibu na Mungu hata watakapokuwa wakubwa. Kutengeneza watoto ambao watakuwa wanajua umuhimu wa maombi, umuhimu wa neno la Mungu juu ya maisha yao , wenye kulijua na wawezao kulitumia katika mazingira yoyote waliyopo. Na ibada hizi uwa msingi imara kwa kanisa pia.

George Barna, anasema wazazi wa “ushindi wa kiroho” upanga dakika 90—120 kwa siku wa kuzungumza na watoto wao, na uweza pungua kutokana na umri wa watoto wanaozungumza nao, na ushauri kutumia mifano hai ambayo ufanana na uhalisia wa maisha ya sasa ili kuwa saidia kuelewa katika mafundisho ya neno la Mungu, hii itawasaidia kujua kuwa neno la Mungu li hai na ufanya kazi hata kwa wakati wa sasa wenye mabadiliko mengi.

1.     Chezeni pamoja (play together)
Kucheza pamoja ni jambo la msingi sana ili kuboresha mahusiano, kucheza pamoja kutasababisha ukaribu kati ya wazazi na watoto, mzazi kwa mzazi na watoto kwa watoto, na kuzidisha upendo, umoja na amani ndani ya familia. Wazazi wengi wamekuwa na mtazamo ya kuwa kucheza pamoja kama familia ni kujidharirisha na kusababisha watoto wamdharau.  

Kielelezo no 10: Mfano wa nafasi ya mzazi kama rafiki kwa mtoto. ©kidzfunonline
Mzazi kutenga muda na kukaa na watoto pamoja na kushiriki michezo kwa pamoja uwa ni njema sana na inawapa uhuru watoto kuwa karibu na wazazi na hata kuwashirikisha mambo mengi, kwenye michezo mioyo ya watoto ufunguka zaidi na ufurahi sana na uweza kuamua kusema mambo mengi sana kwa wazazi wao kutokana na ule ukaribu. Katika michezo pia mzazi anaweza kupata kufahamu moyo wa mtoto/watoto wake upoje/ipoje, wapo katika njia sahihi au isiyo sahihi.

Katika michezo mzazi anaweza kuchekeshana na mtoto, na michezo ipo mingi sana na katika kipengele hiki ujumuisha kutoka nje na kwenda kutembea pamoja katika sehemu mbalimbali na kutazama vitu mbalimbali na kufurahi pamoja na hata kushiriki chakula kwa pamoja. Hii itamtofautishia ukaribu wako kwake na marafiki wengine na itakuwa usalama sana kwake kama ni binti wakati wa kuchumbiwa utakapokaribia hatochanganywa na kudanganywa na vitu kama hivyo kwa kuwa alikuwa ameshaanza kuvipata toka kwa wazazi wake.
2.     Pangeni pamoja (plan together)
Familia nyingi zimekuwa na tabia ya kuwaondoa watoto katika maamuzi mengi ya familia na watoto wengine si wadogo katika kufanya maamuzi ila hawashirikishwi katika kufanya maamuzi. Suala hili limekuwa ni tatizo kubwa katika makuzi ya mtoto na pia uondoa ujasiri na kujiamini kwa mtoto.
Kielelezo no 11: Mfano wa wana familia wakiwa katika kupanga pamoja ©Radical Survivalism
Ni busara kwa wazazi kuwashirikisha watoto wao ambao wamekuwa wakubwa katika maamuzi mengi yanayofanyika katika familia na kuwa na vikao kabisa katika familia kuangalia kutatua na kupanga mambo mbali mbali ya msingi yanayopaswa kufanyika katika familia. Licha ya kuwaongezea ujasiri na kujiaamini watoto, ila pia inapanua ufahamu wao kuhusu maisha na kuwaongezea maarifa mengi kuhusu maisha, na hupata  nafasi ya kujifunza mambo mengi ya maisha ambayo nyinyi wazazi kama viongozi huyafanya. 
Ushiriki wao katika maamuzi mbalimbali uwajengea sana hali ya kujiamini hata kuwa watofauti sana wawapo na wengine, na uwafanya kuwa na upeo mkubwa wa kufikiria na kufanya maamuzi na zaidi kwa kuwapa nafasi unaandaa viongozi bora katika jamii na hata familia zao wenyewe.

3.     Fanyeni pamoja (perform together)
Mbali na mambo hayo matatu lipo jambo kubwa pia ambalo linahusu kufanya pamoja na kwa ushirika, hii pia uongeza umoja na mshikamano katika familia, kwa mfano eneo la kula wababa wengi hupenda kula peke yao na kutengewa chakula mbali na watoto, kwa kufanya hivi tabaka katika familia uweza tokea; lakini kukaa pamoja na kula pamoja katika familia huleta ukaribu na hata kujenga urafiki katika familia.
Zipo kazi nyingine za mikono kama kupika, kuosha vyombo na nyingine nyingi hupaswa kufanya pamoja na kama utamhurumia kuzifanya unamuangamiza na si kumjenga. Kama mzazi unapofanya pamoja na mtoto unamsaidia kujua yale unayoyajua na unamjengea tabia ya kuweza kujisimamia mwenyewe pale unapokuwa haupo na anaweza akasimamia majukumu yote kama vile uwezavyo wewe kusimamia ukiwepo.

___
Mwalimu Kelvin Kitaso anapatikana kupitia 0767190019 / 0713804078 na pia kupitia barua pepe; kitasokelvin@gmail.com 
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.