SOMO: ROHO YA YEZABELI - ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMASOMO: ROHO YA YEZABELI

Historia ya Yezabeli imeandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa kwanza na wafalme wa pili .kitabu hiki kilikuwa kimoja lakini waandishi walikigawanya sehemu mbili. Kiliandikwa na mfalme ahabu aliyekuwa mfalme mzuri wa Israeli ambaye alioa mke aliyeitwa Yezebeli. Huyu mfalme alikuwa akichochewa na mkewe atende mambo maovu kwa watu na kutoka kwenye kusudi lake.


“(Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana ambaye Yezebeli mkewe alimchochea.” 1Wafalme 21:25

Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke akawaweka hapa duniani na kuwapa majukumu ambapo Baba anakuwa na maono ya falmilia na mwanamke anakuwa msaidizi wa kutimiza maono ya familia kutoka kwa Baba.

“Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria. Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake. Nabothi akamwambia Ahabu, Bwana apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu. Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula. Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula? Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu. Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli. 1 Ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu katika Yezreeli, karibu na nyumba ya kifalme ya Ahabu mfalme wa Samaria. Ahabu akasema na Nabothi, akamwambia, Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake. Nabothi akamwambia Ahabu, Bwana apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu. Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli, akisema, Sitakupa urithi wa baba zangu. Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula. Lakini Yezebeli mkewe akamwendea, akamwambia, Kwa nini roho yako ina huzuni hata usile chakula? Akamwambia, Kwa sababu nimesema na Nabothi Myezreeli, nikamwambia, Unipe shamba lako la mizabibu kwa fedha, au, ukipenda, nitakupa shamba la mizabibu lingine badala yake. Akajibu, Sitakupa shamba langu la mizabibu. Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli.” 1Wafalme 21:1-

Mfalme wa Israeli aliamua kumfuata naboth ili ampe shamba lake naye ampe shamba lingine la mbali ambalo ni zuri au ampe fedha ya thamani ya shamba hilo. Naboth alimjibu huyo mfalme “Bwana na aepushe mbali shamba langu la urithi nilipewa urithi nilioachiwa na Baba yangu” Naboth akakataa kununulika na Mfalme. Mfalme alirudi nyumbani na huzuni ya ajabu sana kwasababu amekataliwa kupewa shamba na Naboth. Mke wa Mfalme alimkuta mumewe akiwa na huzuni ya kukataliwa shamba na naboth, akamwambia kama yeye na Ufalme wake wa nchi mambo madogomadogo kama haya yanakushinda? Amka ule, unywe na mimi nitakupa hilo shamba.

Yule mwanamke akaingia kwenye ofisi ya mumewe na kufanya mpango wa kuinua watu wawili wasiofaa ili wamshitaki na kumshuhudia kunena kuwa amemtukana Mungu na Mfalme, kasha wamchukue nje wakampige kwa mawe mpaka afe.
(Wanawake wana nguvu sababu Mungu alimfanya mtu kwa udongo wa adhi na kutoka kwa mtu huyo akamtengeneza mwanamke. Unaweza kumkuta mwanaume akiwa rafurafu na si jambo la ajabu sana, Mungu aliamua kumuumba mwanamke kutoka kwenye udongo wa mwanaume. Kwa maana nyingine Wanawake wamejengwa na Wanaume wamefyatuliwa. Mungu alitoa material safi akamuumba mwanamke kwahiyo mwanamke anauhai mara mbili, wanawake wana nguvu kubwa ya ushawishi ndiomaana imeandikwa Sulemani mwana wa Daudi alioa wanawake wengi wakaugeuza moyo wake.)

Baadaye huyu Yezebeli alimwamsha mumewe aende akamiliki shamba lake, Mungu aliamua kuingilia kati mpango huu kupitia nabii Eliya mtishibi, Kwenye kila kizazi Mungu huinua mtu kulingana na kizazi chenyewe kilivyo. Kila Mfalme aliyekuja katika Israeli alipakwa mafuta kwaajili ya kazi maalum, Sauli alipakwa mafuta na Bwana kuangamiza waamaleki lakini alishindwa kutimiza kusudi lake akafariki, Mfalme Daudi alipakwa mafuta kwaajili ya kuwaangamiza Wafilisti na alipoingia kwenye Ufalme akawatahiri kwa nguvu Wanaume 450 akaendelea na kusudi lake na akawa Mfalme kwa muda wa miaka 120. Hii inamaana unapokuwa umepewa wito ukautimiza utaishi mika mingi, Mfalme Solomoni alipakwa mafuta ya kujenga nyumba ya Bwana sio kupigana kama wafalme wengine na hakupigana vita zaidi ya mbili, alitumia mbinu ya kuangalia Mfalme mwenye nguvu aliye karibu yake ambao ni Sidomu na Misri na kuwaoa binti zao ili walipotaka kumvamia awaambie wanataka kuwauwa wajukuu zao?, Eliya alipakwa mafuta kwaajili ya kuangamiza nyumba ya Ahabu na kushuhulikia yezebeli na familia yake. kwahiyo kila kizazi na mtu wake wa kukinyoosha na kizazi hichi vilevile Mungu amemuinua mtu kwaajili ya kukinyoosha kikae kwenye mstari.
Wakati Yezebeli na Mumewe Mfalme wanaelekea kumiliki shamba la Naboth Eliya alizuka na kumwambia Mfalme umeua ili utamalaki hivyo utakufa kwa kuliwa na mbwa.

ROHO YA YEZABELI.

Roho ya Yezebeli ni mapepo yaliyo ndani ya mwanamke yanawakontrol wanawake wawatale wanaume kufanya mapenzi ya kishetani.

“ Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi. Yeremia7:18

“Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.” Yeremia 44:17

Roho ya Yezebeli ni mashetani ya ustawi ambayo yanakaa angani na kwenye Biblia yanaitwa atemi waefeso, sainbere au mama mtakatifu ndio huyohuyo yezebeli na kazi yao ni kumiliki uzazi.

Imeandikwa “Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi” Waefeso 2:2

Huyu mwanamke yezebeli alikuwa akiketi kwenye meza ya chakula na wanaume 400 upande wake wa kulia na 400 upande wake wa kushoto, kazi ya mwanamke huyu ilikuwa ni kuwaua manabii wa Mungu, Obadia alikuwa anafanya kazi kwa Mfalme wakati huo alikuwa akiwachukua wachungaji na kuwahifadhi chini ya mapango sababu ya kumwogopa yezebeli asiwauwe. Hapa tunajifunza kwamba kuna wachungaji wa aina mbili aina moja ni wale wanaojificha kumwogopa Yezebeli na wengine ni wale walio kwenye operesheni kumkabili Yezebeli na kumfyatulia mbali kama Eliya mtishibi.

Elia alikuwa amejificha mahali akiomba na akaamua kujitokeza kumkabili Yezebeli. Imeandikwa “Ingawa tunaenenda kwa jinsi ya Mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya Mwili kwamaana silaha za vita vyetu zinauwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.”
Ule wakati wa kulala ndani ya pango umekwisha sasa ni wakati wa kutoka mbele na kupigana vita kukabiliana na Yezebeli. Mungu ameweka Obadia kila mahali kwaajili ya kuleta taarifa zinazoendelea na wakati Obadia analeta taarifa Elia mtishibi anatoka na kukabiliana nao.

Imeandikwa “Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.” 2Wafalme 6:16

Imeandikwa “Wale washindanao na Bwana watapondwa kabisa”. Watumishi wa Bwana walipokuwa mapangoni Obadia hakuogopa kutoka Ikulu ya mfalme kuwapelekea vyakula manabii sababu Yezebeli alikuwa ameshikilia msimamo wa kuwauwa popote pale wanapoonekana.

“Kulikuwa na jitu lilinyanganywa viatu, lilipigwa sindano ya usingizi likalala lakini Mungu wa Mbinguni akaliangalia lile jitu akaona ameweka uwezo ndani yake lakini limelala. Mungu ameamua kuliamsha lile jitu nalo limeamka limejitikisa na kuangalia limenyanganywa viatu na kufungwa na lilipoangalia limeona lina uwezo wa kuanza safari bila viatu na limekwisha kuanza safari yake na linaenda kuteka Dunia nzima kwa uwezo wa ajabu na Jitu hilo ni kanisa.”

Elia aliamua kwenda kumfuata Ahabu kwa kuonana naye, Hapa tunajifunza kwamba kuna wakati wa kupigana vita ukiwa kwenye maombi na wakati wa kupigana mwilini, Yesu aliposikia anatafutwa na herode aliamua kukimbia, siku moja Yesu alibebwa ili asukumwe kwenye bonde na akaamua kupita katikati yao na kuondoka, siku moja aliamua kuingia hekaluni na kukuta watu wanafanya biashara akachukua kikoto(kamba yenye kanundu mbele) na kuwapiga wafanya biashara wote na kuondoa biashara zao huku akiwa mwenyewe Saa ya kuwapiga ikifika wote wanakuwa wamenyauka.

Walinzi wa Milango

Ni vizuri ujue jambo moja kwamba kuna walinzi wa milango wapo wanatenda kazi, zamani miji inapojengwa ilikuwa ikizungukwa kwa ukuta na kunakuwa na walinzi wameilinda kwenye malango yake, ukisoma kwenye Biblia Yerusalemu ilikuwa imezungukwa na Ukuta, Malaika walipokwenda sodoma na gomora Ruthu alikuwa mlinzi wa lango na alikuwa na macho ya rohoni alipowaona akawatambua ni malaika hivyo akawachukua hadi nyumbani kwake. Kwenye ulimwengu wa rohoni kuna walinzi wa ngome ambao wanakuwa wamekaa ndani ya mtu ambao ni mapepo na yanakuwa yanajua leo kanisani kutakuwa na neno la ajabu na wewe utafunguka wanakufanya ukitaka kwenda kanisani tu anakuja mgeni nyumbani kwako hivyo unashindwa kwenda kanisani, walinzi wa ngome wengine ukifika kanisani tu mahubiri yakianza unaanzasikia kichwa kinauma na unajisikia kuondoka kwenye ibada, walinzi wa ngome wengine wanakupa usingizi wa ajbu kama bulletproof ya kutokusikiliza somo sababu usiposikia Neno kawaida huwezi kufunguka matatizo yako, walinzi wa ngome wengine wanakaa kwenye vinywa unaweza ukamkuta mtu anatabia ya kuropoka vitu vya ajabu toka kinywani mwake na ukimchunguza mtu huyo utagundua anakosa vitu vingi sababu ya kinywa chake kimejaa walinzo wa ngome.

Tanzania yenyewe imelindwa na walinzi wa ngome kusiwe na mlipuko wa Mungu, Askofu Emanueli Lazaro na Moses Kulora walikuwa wanahubiri kwa kasi ya ajabu siku za nyuma na watu wa usalama wakafanya mambo ya kuwagawa ili kasi yao ipungue kusiwe na nguvu za Mungu sababu baadhi ya watu wamekwisha kuweka mambo yao yasiharibik. Mungu aliamua kufungua mlango mwingine baada ya mpango wa kuwagawa kina Emanuel Lazaro na Moses kulora wakawa wanahubiri kila mtu kivyake na bado kanisa likasimama kwa namna ya ajabu, Leo hii Ufufuo na Uzima imesimama kwa nguvu za ajabu ni mtu mmoja ambaye amekusanyika kama watu wengi wanatenda kazi kwa pamoja kwa nguvu za Mungu aliye hai ndani yao.

Hii ni saa yetu na saa ikifika imefika hakuna wa kuizuia.
Baada ya Elia kutenda kazi Mungu alimuinua Yehu aliyepewa uwezo wa kumfyeka Yezebeli. Yehu alisema manabii wa baali wote na wasoma nyota wote, waganga wote, wachawi wote waje bila kukosa hata mmoja nataka kuwapa heshima, walipoingia alifanya msako wa manabii wa Jehova walioingia ndani ili waondoke nje. Walipotolewa wote Yehu alitoa amri ya kukatwa vichwa mpaka wote wakauwawa na maandiko yaasema hivi ndivyo Mungu alivyowaangamiza manabii wa mungu baali, alipomaliza alielekea kwa mwanamke Yezebeli ambapo yezebeli alipomwona aliingia ndani kujiremba Yehu akamwambia atoke nje na alimkanyaga kichwa na kumuuwa. Baadaye Yehu akaagiza watoto wa uzao wa Yezebeli wakatwe vichwa vyao na kumpelekea Yehu.

Ukishinda kwenye ulimwengu wa rohini utashinda kwenye ulimwengu wa mwilini na Ukifika wakati anayeumba ameonekana ujue mwisho umefika.

Ninaamuru kwa jina la Yesu kristo roho ya yezebeli inayoandama ndoa yangu, kazi yangu, maisha yangu ianguke kwa jina la Yesu kila roho ya yezebeli inayofanya kazi ndani ya Tanzania naikatilia mbali kwa jina la Yesu. Walinzo wa ngome wanaonizuia kwenye ndoa, kumiliki kazi, biashara zangu, elimu yangu, kazi yangu ninawaangamiza kwa damu ya mwanakondoo Yesu kristo. Amen
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.