SOMO: TANGU LEO MTU ASILE MATUNDA KWAKO - ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA


SOMO: TANGU LEO MTU ASILE MATUNDA KWAKO

“Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia. Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazama, mtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.” Marko 11:12 – 14, 21 - 25


Yesu aliona njaa akaona mtini una majani akauendea ili apate chochote cha kula lakini wakati ule ulikuwa sio wakati wa mti ule kuzaa matunda na akauambia ule mtini tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Muda huo ulikuwa ni asubuhi na kesho yake alipokuwa anapita eneo lile wanafunzi wake waliuona mti ule umenyauka toka shinani na Petro akamwambia Yesu kana kwamba hajui lililotokea kwamba mti ule umenyauka lakini Yesu akamwambia mwaminini Bwana.

Kwa habai hii Yesu alikuwa anafundisha ulimwengu wa roho. Mti ule ulilaaniwa asubuhi na kesho yake asubuhi ukaonekana umeshakauka. Hii inatufundisha kwamba jambo linaposemwa linafanyika muda uleule kwenye ulimwengu wa roho na baadaye linakuja kudhihirika kwenye Ulimwengu wa mwilini. Kuna ulimwengu wa aina mbili, ulimwengu wa rohoni(usioshikika) na wa mwilini(unaoshikika). Mtu anapokufa anakufa kwenye ulimwengu wa roho kwanza na baadaye anakuja kudhihirika kwenye ulimwengu wa mwili, kitu chochote huanza kufanyika kwenye ulimwengu wa roho kwanza na baadaye kinadhihirika kwenye ulimwengu wa mwili. Tumeona Yesu ametamka maneno na mti ule ukanyauka tangu muda alipotamka lile neno na kesho yake ukatokea mwilini. Yesu alijua jambo lile limeshafanyika tayari lakini alijipitisha mahali pale kana kwamba hajui lililofanyika ili awafundishe wanafunzi wake kanuni hiyo.

“Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.” Yohana 9:1-30

Hayo maisha magumu na hali unayoipitia usifikiri Mungu amekuacha au umetenda dhambi bali unatakiwa ujue lipo jambo Mungu anataka kutenda . Mtu mmoja kipofu tangu kuzaliwa alikutana na Yesu akamponya macho yake. Yale maneno aliyotamkiwa na Yesu ya kwenda kwenye maji ya siloamu tayari ulikua ni uponyaji kwa kipofu Yule japo ilimpasa aende kwenye maji kulithibitisha lililosemwa kitokee katika ulimwengu wa mwili.

1Wafalme 22:28

Mungu amekuumba wewe kwa vipande vitatu ambavyo ni roho, nafsi na mwili. Mungu anakaa ndani ya Roho yako unapokuwa unanena kwa Lugha Mungu anatoka rohoni na kuingia mwilini na kila mtu ndani yake Mungu zipo nguvu za Mungu imeandikwa;
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo” Waefeso 1:3

Ukiri:
“Mungu amenibariki Baraka zote kwenye Ulimwengu wa roho”

“Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu. Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.” 2Petro 1-13

Uwezo huu umedhihirishwa kwenye ulimwengu wa roho na Mungu ameshatoka rohoni ameingia mwilini na lolote unalolisema linakuwa vilevile sababu siyo mtu anayezungumza bali ni Mungu anazungumza kupitia mwanadamu.Imeandikwa;
Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.

1Wakolosai 1:24

Mungu amekaa ndani yako na nguvu zake na uweza wake lakini yupo rohoni amekaa na anataka atoke kupitia wewe tokea nafsini mwako. Mtu wa Mungu akitamka neno kwaajili yako kwenye ulimwengu wa rohoni lile neno linaanza kusababisha matukio mpaka linakuja kutokea mwilini. Ndio maana Mungu akasema neno lake halitarudi bure mpaka limetimiza makusudi yaliokusudiwa. Imeandikwa;

Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. Waebrania 4:12-13

“Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida” Matendo 19:11

Bwana akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.
1Samweli 3:11

“Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia? Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.” Isaya 43:13, 19

Mungu amemuumba mtu vipande vitatu, cha kwanza ni mtu mwenyewe ambaye ni roho, kipande cha pili ni nafsi (kujisikia, nia, utashi) na cha tatu ni mwili. Namna ya kutembea, kuhisi, kupenda au kutopenda au ukiamua kwenda baa na kulewa au kufanya uzinzi na uasherati, ukiamua kutukana, ukiamua kuzira na maamuzi mengine huo ni utashi wa mtu ambao ameamua kupitia nafsi yake na Mungu amewapa wanadamu uwezo wa kuamua wenyewe kwa kutumia utashi wao bila kuwaingilia na usitegeme hata siku moja Mungu atakuja kwako kukukataza usiende kufanya uinzi sababu ni wewe mwenyewe na uhuru wa utashi wako ulionao umekupa maamuzi hayo,maana alivyo mtu nafsini ndivyo alivyo yeye.

Hisia za mtu zinamfanya mtu kuwa sehemu ya yeye vinakuwa sehemu ya maisha yake, utashi wa kufanya kitu mara kwa mara itafika wakati kile kitu kunahama kwenye hisia na kuingia ndani ya maisha ya mtu mwenyewe.

Kupitia unachoona kusikia, kuonja, kugusa, dunia inaingia na inajaa kwenye nafsi na wakati unanena kwa lugha Mungu anakuwa yupo rohoni na anataka atoke aingie mwilini adhihirike kwa watu kwa kutenda miujiza ya uwezo wake anashindwa sababu ya mazagazaga ya yaliyohifadhiwa ndani ya nafsi yako.

Kwamaana imeandikwa tunaenenda katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili kwamaana silaha za vita vyetu zinanguvu katika mwili hata kuangusha ngome. Ngome zinazozungumziwa hapa ni yale mazagazaga ya tabia ya kupenda picha za ngono, kuongea matusi, uongo, wivu, masengenyo, umbea, uchochezi, uonevu, wizi, tabia mbaya, dharau, husuda, na mambo mengine kama hayo yanaitwa mazagazaga na ndio yanayomfanya mtu ashindwe kutokeza nje ya dunia ili aseme kupitia mtu Yule, aponye kupitia mikono ya mtu huyo, akemee kupitia mtu, abariki kupitia mtu unakuta mtu anaye Mungu ndani yake lakini hawezi kutokeza nje na kudhihirika kwa watu sababu ya mazagazaga hayo
Nafsi yako ikiwa safi Mungu anajidhihirisha na kutenda kazi, unaweza kumwangalia mtu akadondoka chini kwamaana hakuoni wewe bali anamwona Mungu ndani yako, Yesu aliendewa na kipofu na akamwomba kama akitaka anaweza kumtakasa na Yesu akamjibu nataka takasika, sababu nia yake, nafsi yake imeendana na nafsi ya Mungu hivyo Yule kipofu wa kuzaliwa akapona saa ileile. Elimu za kidunia zinaweza kumzuia Mungu asitoke rohoni na kupita nafsini sababu nafsi imejiunganisha na mazagazaga ya elimu ya duniani.

“Uwezo wako wa kuyaondoa mazagazaga ndio uwezekano wako wa kudhihirisha nguvu za Mungu”

“Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.” Waebrania 9:22

Moyo, Nafsi, Utashi vyote hivi vinasafishwa kwa damu. Inakupasa kusafisha nafsi yako kwa damu ya mwanakondoo ili kuondoa mazagazaga ambayo ndiyo yanayozuia Mungu kutenda kazi kupitia mwili wako mfano mikono yako, sauti hata kivuli chako.
Naamuru mti usiozaa matunda uliopandwa katika nchi ya Tanzania ukauke kwa jina la Yesu.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.