SOMO: UTOSHELEVU WA NDANI HUAMUA MAMBO MENGI YA NJENa Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

UTOSHELEVU WA NDANI HUAMUA MAMBO MENGI YA NJE
Utoshelevu ni neno linalotokana na na neno kutosheka,kutosheka ni hali ya kuridhika na kile ulichonacho kwa wakati husika ulio nao.Kuridhika na jambo haimanishi kwamba ndio ufikie mwisho wa kuendelea mbele juu ya jambo unalohitaji bali kuridhika kunakupa mwanya mpana wa kutazama mambo kwa upana wake bila kuwa na hisia zilizojawa na mihemko.

Kuridhika jambo kutakusaidia zaidi kuwa na kiasi kwenye mambo mengi bila kuleta/kupata uharibifu usiokuwa na ulazima. Kuna uwezekano kukawa na aina nyingi za utoshelevu ambazo mtu anaweza kuzipata kulingana na mambo kadha wa kadha anayoweza kuyafanya lakini utoshelevu wowote ule wa jambo lolote lile usipoanzia ndani ya moyo wa mtu huyo masumbuko na kutoridhika katika kile akifanyacho huwa makubwa. Ili kupata utoshelevu wa ndani kwenye kila jambo ni lazima utambue ni vitu gani vinaweza kukusaidia kuwa na utoshelevu wa ndani na vitu gani vinatokea pale utoshelevu wa ndani unapokosekana katika kile ambacho unaweza kuwa unakifanya. Kwanza Kabla Haujamua kufanya Jambo lolote ni lazima utambue uwezo wa nguvu ulizo nazo na Udhaifu ulio nao kwenye kile ambacho unahitaji kukifanya.

Mara nyingi kwenye maisha yetu kuna aina ya kwanza ya changamoto ambayo huwa tunakutana nayo ni ile inayochangiwa na maamuzi yetu binafsi tulio nayo kwenye jambo husika bila muingiliano wa jambo lolote kutoka nje.Kutokutambua athari na matokeo ya maamuzi binafsi unayoyafanya kunaweza kukakuondolea utoshelevu wa ndani.Maamuzi yoyote yale kwenye maisha yako mara nyingi hucheza katikati ya Nguvu na Uwezo ulio nao juu ya jambo unalolifanyia maamuzi lakini pia udhaifu ulio nao juu ya jambo ambalo unalifanyia maamuzi .

Maamuzi yoyote yakizidi uwezo na nguvu ulizo nazo maana yake yataenda kuangukia kwenye udhaifu ulio nao na matokeo yake hautapata matarajio husika nah ii itapelekea wewe kutopata matokeo uliyoyatarajia na kuharibu lile changamko la moyo ambalo kwa kiasi kikubwa husaidia kuimarisha utoshelevu na kuridhika kwa moyo wako. Pili Lazima utambue mazingira yanayokuzunguka kabla ya kufanya uamuzi wowote ule.Unapoamua kufanya maamuzi yoyote bila kujua aina ya mazingira ulio nayo inakujengea uwanda mpana wa moyo wako kufadhaika na mwisho wa siku moyo husinyaa na kupelekea changamko la moyo kupotea mwisho wa siku ule utoshelevu na kuridhika kwa moyo hupotea kabisa.

Kuna changamoto nyingine zinazokuja kwenye maisha yetu husababishwa na sababu za nje yetu wenyewe,muda mwingine changamoto hizi haijalishi umefanya\haukufanya maamuzi hayo bado zitakuja tu.Imekupasa kuyatambua mazingira kama haya ili hata pindi litakapotokea lisiwe kikwazo cha wewe kukosa utoshelevu wako wa ndani na furaha yako ya ndani ambayo baadae hupelekea wewe kuyafurahia maisha kwa namna moja au nyingine. Utoshelevu wa ndani wa mtu unapokosekana kila analolifanya kwake ataliona kana kwamba halikidhi kiu na haja ya moyo wake na mwisho wa siku mtu huishia kutanga tanga na hushika hiki na kuacha kile na kufanya hiki na kufanya kile.

Ni muhimu sana kuhakikisha unajenga stamina ya ewe kuwa na uwezo wa kuhakikisha utoshelevu wako kwenye mambo mengi uanzie ndani ili kuweza kukusadia na kukufanya uyafurahie maisha.Kulaumu kwako au kusononeka kunaweza kusilete matokeo yalotarajiwa lakina unapojenga uwezo wa kutosheka kutoka ndani pia unatoa uwanda mpana wa akili yako kufanya kazi kwa ufasaha na upana zaidi bila kuchoka lakini pia akili yako itafurahia matokeo ya kile ambacho unaweza kufanya. Ukiona kila unachotaka kukifanya hakikupi utoshelevu wa ndani basi usijisumbue kiache kukifanya na tafuta kitu ambacho kinaweza kukupa utoshelevu wa ndani usilazimishe kwa sababu imekulazimu kukifanya bali hakikisha moyo wako unapata changamko na furaha ya kweli ya ndani.Utakapolazimisha kukifanya mara nyingi hata kama utafikia kilele cha kufanikiwa lakini bado lile changamko la kweli la ndani halitakuwepo kabisa.

“UTOSHELEVU WA NDANI HUAMUA MAMBO MENGI YA NJE” E-mail: naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless You All
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.