SOMO: UWEZO WA NGUVU ILIYO NDANI YAKO


Na King Sam

UWEZO WA NGUVU ILIYO NDANI YAKO
Waefeso Ephesians 3:20
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

Kila Mtu aliyeitwa na Yesu (kuokoka),amepewa kitu kulingana na Uwezo wa Nguvu iliyo ndani yake,
Ili limekuwa tatizo kwa mwili wa Kristo watu kutokujuwa kila mmoja amepokea kulingana na Uwezo wa nguvu itendayo kazi ndani yake,
-Iwe ni Biashara
-Iwe ni huduma kila Mtu amepewa kulingana na Nguvu ya utendaji kazi ndani yake,
Kile ntakachokuonyesha leo kitabadilisha maisha yako,nacho ni Uwezo wa utendaji ndani yako,ndiyo maana ukiona watu wanafanikiwa unafikiri kuna njia nyingine wanatumia,ni kweli kuna watu wanapokea rushwa kuna watu wanatumia uchawi lakini hao hawadumu wala Mali zao hazidumu kwa hiyo wewe usijali kuhusu hao,nachoongelea ni wewe uliyechaguliwa na Yesu akakupa kitu cha wewe kuzalisha.

KUNA WATU WANAFIKIRI WENGINE WAMEPENDELEWA
Hakuna Mtu aliyependelewa Bali ni
Biblia inasema hivi...
Mathayo Matthew 25:14
Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; KILA MTU KWA KADIRI YA UWEZO WAKE; akasafiri,

Mfano huu ni Yesu unaona hakutumia upendeleo Kama vile wengine katika maisha yao wanafikiri watu katika mafanikio wamependelewa,hakuna kitu kama hicho hata uwe na kiasi gani cha pesa zinaweza kuzaa kulingana na Uwezo wa kufikiria ndani yako,kama kufikiri kwako ni kushindwa utashindwa tu,
Kama kufikiri kwako ni kuweza utaweza tu hata Kama kuna vizuizi mbele yako,
Haijalishi ni Biashara inaweza kufanikiwa tu kulingana na Uwezo wako ndani yako na ndiyo huo Uwezo utasababisha uzalishe ili ufanikiwe,

ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAYEFANYIA KAZI KILE ULICHOPEWA
Kama kunakitu unachoitaji kutafuta ni ROHO MTAKATIFU yeye ndiye anafanya kazi ndani yako,kile Mungu alichoweka ndani yako ili kizae unaitaji Roho matakatifu la sivyo utakuwa unaogopa kufanyia kazi huo mtaji wako,au utaona unaitaji mtaji mkubwa ili ufanye Biashara au utaona hiyo kazi hailipi Bali unaitaji kazi nyingine,
Ndugu yangu Roho mtakatifu ndiye mwalimu wetu kutufundisha kutumia kile tulichopewa,kutuongoza hata kama ulichopewa ni talanta moja Roho anakufundisha kuizalisha

Haupo duniani kwa hasara umeumbwa kwa kusudi
Angalia mstari wa 7
Isaya Isaiah 43:5
Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;
6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.
7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.

Unaweza kuwa mahali popote ukafanikiwa inategemea na Uwezo wa kufikiri kwako ndani yako,tabiriwa utabiriwavyo,ombewa uombewavyo Kama ndani yako hakuna nguvu ya kukuonyesha ushindi,huwezi kushinda,ndiyo maana unaona watu wanaombewa na maisha hayabadiliki tatizo ni wewe kuona uwezi inasema uchumi umeharibika ni wewe kuwa na tabia ya kuchagua kazi nk

Kila siku nasema shida si kazi uliyona, shida si biashara uliyo, shida si mtaji ulionayo shida ni wewe kama leo ukijuwa kulingana na Uwezo ulionao ndani yako umepokea ulichonacho unaweza kuzalisha
Biblia inasema hivi..
Zaburi Psalms 1:3
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Ukienda bank unaweza kuona watu wanakwenda kukopa kulingana na Uwezo wa nguvu inayotenda kazi ndani yao ya kufanya hiyo Biashara wanayo kwenda kuikopea pesa,
Kwa nini mmoja anakopa milioni miamoja
Kwa nini mwingine anakopa milioni kumi
Na kwa nini mwingine anakopa milioni moja
Kila mmoja anawaza kwa jinsi atakavyoweza kurudisha, swala hapa si kurudisha swala ni Uwezo wa kuweza kuzalisha na kurudisha huo mkono ndiyo umemsukuma kukopa kiasi hicho,

Kwa hiyo ndugu zangu katika Kristo Yesu usiwe na wivu bali juwa Kila mmoja amepewa kulingana na Uwezo ndani yake,kile unachofanya fanya kwa bidii utafikia malengo yako,maana kila mmoja anamalengo yake kutokana na Uwezo wake ndani yake,Mtu asikudharau kwa kile unachofanya,na usimonee mwenzako jicho ni kutokana na Uwezo wake ndani yake.

Talanta uliyopewa inaweza kuzaa na kukusababisha malengo yako kutimia umepewa hiyo kutokana na Uwezo wako wa kuzalisha uwezi pewa tano wakati hauna Uwezo wa kuzizalisha uwezi ndiyo maana watu wanakufa kwa presha kwa wizi ukahaba wakitafuta vilivyo juu ya Uwezo wao.

Omba upate Roho mtakatifu akuwezeshe kuzalisha kile ulichopewa katika jina la Yesu amen.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.