UJUMBE: KUWA KAMA FLANI - KING SAM

Mfano wa kijana upande wa kuume aliyetaka kuwa kama mwimbaji anayempenda©buzznewsworthy
KUWA KAMA FLANI
Musa,Joshua,Yohana,Yesu
Hiki ndicho kitu kinatesa kanisa na ulimwengu pia,
Ntaongelea wanaotaka kuwa Kama flani katika Roho na pili wanaotaka kuwa kama flani katika Mwili
Nianze kwa kusema hivi umezaliwa kwa KUSUDI wewe mwenyewe na mwingine hivyo uwezi kuwa Kama flani,labda unaweza kumzidi au unaweza kuwa chini kuliko yeye iwe ni kwenye huduma au Biashara au kwenye familia na hata kwenye Ndoa pia.

1 Wakorintho 1 Corinthians 12:4
Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.
5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

Kila Mtu kumbuka amezaliwa kutimiza kusudi la Mungu juu yake hapa duniani ndiyo maana unaitaji kujuwa uwezi kuwa Kama flani Kama ungekuwa basi kusingekuwa na sababu ya yeye kuwapo au na maana ya yeye kuwepo hapa duniani,
Ndiyo maana unaona kunatofauti kati ya Yohana mbatizaji na Yesu Kristo,Yohana anaitajika kwa kazi aitengeneze njia kabla ya kuja kwake Yesu,maana anachokuja kufanya Yesu si kile atakachofanya Yohana,

Dambi iliingizwa duniani na Adamu lakini anaitajika Adam mwingine kumtoa Mtu kwenye dhambi au mauti iliyoingizwa na mwingine kwa nini Mungu hakumtumia huyo huyo aliyeingiza atoe au awatoe huko?ndiyo ujuwe hivyo,upo wewe Kama wewe kwa kusudi
Waroma Romans 5:12
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Kuna mambo wanafunzi walitaka Yesu afanye ya kuita moto Kama Eliya lakini kumbe hawakujuwa Eliya alikuwa na kusudi lake na Yesu alikuwa na kusudi lake,kusingekuwa na maana basi Eliya kuwepo au Yesu kuja
Luka Luke 9:54
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.

Kwa hiyo Kama unaweza kufanana na flani unawaza vibaya unauwezo wa kumzidi au kutomzidi lakini uwezi kuwa Kama Yeye maana ni Yeye tu amekuja kwa kusudi ilo,unaona hata ugunduzi wa vitu kama magari ndege matrani na meli walio gundua walikuwa wao tu hawa wengine watakuwa ni kufanya kuwa vya kisasa zaidi kutokana na majira Lakini mgunduzi alikuwa mwingine
Mhubiri Ecclesiastes 1:9
Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.
Kuna watu wanafunga na kuomba ili wagunduwe ndege wewe Ndege zilishakuwepo utakacho pewa ni jinsi gani ya kufanya kiwe cha kisasa zaidi,

Angalia Yesu anachosema hapa siyo tu alichofanya utafanya hata kile hukufanya utafanya wewe cha Mlima kung'oka maana wewe utafanya zaidi yake,
Mathayo Matthew 21:21 Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka.

Kwa nini kila mtu atasimama kwenye kiti cha hukumu mbele za Mungu kwa nini kama ungekuwa kama baba yako au mtoto wako angesimama kwa ajili yako?kwa sababu haupo kama yeye kila mtu atahukumiwa kwa kazi yake,na matendo yake,

Ili tatizo limekuwa baya hata kwa watumishi wanataka mafuta kama flani ndivyo hivyo hata kwenye ndoa mwanamke anataka mme wake awe kama mme wa flani mmekwisha hawezi eti hata kufanya kama flani ndiyo maana wanawake wengi wanasikiliza watu nje au wakwe wakisema mme wako angefanya kama mme wa flani au angejitoa kama flani,sasa wewe unataka mme wako afanane na flani kwa matendo au kazi hujui kwa nini umeolewa na yeye basi Mungu hasingekupa huyo,

Hata kwenye kwaya huwezi kuwa kama flani utacopi tu lakini uwezi kuwa kila mtu amebeba kusudi lake wewe ukitakuwa Kama flani utajijuwa mwenyewe wengine wanatumia nguvu za shetani
Tafuta kuwa Kama wewe si Kama flani hata watoto wako hawawezi kuwa Kama wa flani kamwe wale wamezaliwa kwa makusudi yao na wa kwako kwa makusudi yao pia,

Musa yupo kutoa Israel Misri Joshua yupo kuwaingiza nchi ya ahadi hawa ni watu wawili tofauti kiutendaji...badilika katika jina la Yesu.King Sam
Kama unataka niwasiliane na wewe kwenye simu namba yangu hii hapa +447903180067

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.