UJUMBE: USIPOOMBEA UCHAGUZI 2015, NI NANI ATAKAYEKUSAIDIA KUOMBEA?


Na Mchungaji Gasper Madumla

Bwana Yesu asifiwe…

Mtu mmoja aliniambia kwamba ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu tar.25.10.2015 nihakikishe nimenunua vyakula vyote,kwa sababu mara baadaya hapo sitaweza kwenda tena sokoni wala watu hawataweza kwenda sokoni kwa maana kutakuwa na machafuko ya kukosekana na amani kila kona ya Tanzania. Haya yalikuwa mawazo ya mtanzania mmoja,si unajua tena kipindi cha uchaguzi kama hiki,mengi yanaongelewa,kila mtu anaongea analolitaka.

Bali mimi nalimuambia hakutatokea vita ~ bali tuzidi kuomba amani katika taifa letu la Tanzania.

▪ Jukumu la kuombea amani ya taifa letu lipo mikononi mwako mpendwa. Ujue usipoomba, itakuwa ni vigumu akatoka mtu wa taifa jingine akaomba amani ya taifa lako.

Kumbuka;tunahitaji amani tu. Yaani ni hivi,iwe ni rais atoke katika chama tawala au pinzani,lakini kikubwa ni amani itawale. Yule ambaye amekusudiwa na Mungu atawale Tanzania kwa nafasi ya urais awe ametoka kwa BWANA.

Pasipo kuomba,kamwe hatuwezi kumjua kiongozi ambaye chaguo la Mungu. Watu wengi uangalia muonekano wa nje wa wagombea pasipo kuwapima roho zao kwamba zitatunufaisha sisi? Na hapa pana mfano wa wana wa Yese,~Eliabu &Daudi,watu waliopimwa kwanza kwa mionekano yao ya nje kisha Mungu kumbe hapimi hivyo kama mwanadamu apimavyo,bali Yeye BWANA huangalia moyo;

“ Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.

Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo. ” 1 Samweli 16:6-7

Samweli aliweza kuangalia uso,urefu na kimo cha Eliabu akalidhika naye maana alivutiwa na muonekano wake wa nje. Kisha akamsaizi Eliabu kama vile ndio mfalme na kujilidhisha akasema Yakini masihi wa BWANA yupo mbele zake. Kumbe Eliabu hakuwa chaguo la Mungu,bali Daudi haswaa ndie aliyekuwa chaguo.

Muonekano wa nje wa Daudi haukuwa mzuri,sio wa kuvutia kiasi kwamba ndio awe mfalme. Lakini kumbe roho yake (Daudi ) ndio ilikuwa ni bora zaidi ya kaka yake Eliabu.

Katika mazingira hayo,ikiwa hautaomba/hautaongozwa na Roho wa Bwana Yeye aichunguzaye mioyo ya wanadamu basi ni dhahili waweza kumuona fulani anafaa zaidi kuliko mwingine labda kwa sababu ya muonekano wake wa nje.

▪ Kumbe hatuwezi kumchagua kiongozi bora ikiwa kama hatutaomba. Maombi ndio pekee yenye majibu kwa yule mwenye ubora wa kuiongoza Tanzania yetu. Mkristo,umepewa kazi ya kuombea uchaguzi huu,usiwaachie wengine kazi hii,ni kazi yako sasa ya kuombea taifa. Tunataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ni uchaguzi wa amani,lakini pia apatikanike kiongozi mzalendo mwenye kujua maslai ya watanzania wote.

Usipoomba leo,watu wajanja wajanja wenye hila mbaya watamuweka kiongozi wamtakao wao tena wengine watatumia hata kwa njia ya ushirikina kuakikisha matakwa yao yanatimia. Amka na uombee uchaguzi 2015.

Kwa huduma ya maombezi nipigie 0655111149.

Mchungaji Gasper Madumla.

Beroya bible fellowship church.(Kimara,Dar,TZ)

UBARIKIWE.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.