FAIDA CHACHE UNAZOWEZA KUPATA KWA KUWEKA MIPANGO YAKO BINAFSI KWENYE MAANDISHI


Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.


I. MPANGILIO MZURI WA MAISHA BINAFSI.

Mara nyingi watu wenye tabia ya kuweka maisha na mipango yao kwenye maandishi wanakuwa na mpangilio mzuri na wenye tija kwenye maisha yao binfsi.Unapoweka maisha yako na mipango yako kwenye maandishi inakusaidia kutambua ubora wa mipango na udhaifu wa kile unachotarajia kukifanya kwenye maisha yako binafsi. Unapoweka mpango wako kwenye maandishi ni ishara ya kwamba unajitambua na unajielewa na unafahamu kitu gani unahitaji kwenye maisha yako binafsi .Mara nyingi watu ambao wanaishi maisha yasiyokuwa na mpangilio ni watu ambao hata ukichunguza kwa ukaribu utagundua si watu wa kuweka maisha na mipango yao kwenye maandishi mara kwa mara. Maandishi hukusaidia kupiga hatua kwa haraka zaidi kwenye kile unachotarajia kukifanya.Kuweka mipango yako kwenye maandishi ni hatua ya mwanzo na muhimu ya kukuwezesha kupata ushindi kwenye maisha yako binafsi na malengo/mipango uliyokuwa nayo.

2. HAMASA YA MAISHA HUONGEZEKA

Maandishi ni kumbukumbu isiyodanganya ,Unapojijengea utaratibu wa kuweka mipango yako kwenye maandishi inakusaidia kukuongezea hamasa sababu maandishi hayo yatakusaidia kujua iwapo unasonga mbele au unarudi nyuma Hii itakusaidia kutambua wapi unapaswa kuboresha zaidi namna unavyoendesha maisha yako kuelekea ndoto zako muhimu kwenye maisha yako ya kila siku.Muhimu kutambua kwamba maisha yasiyo na maandishi mara nyingi hayana hatua kubwa na maendeleo ya kueleweka maana hauna kitu ambacho kinakupa mwelekeo. Kuandika mipango yako kutakusidia kutambua iwapo unaelekea uelekeo sahihi au unapotea .Ni ngumu kujua unapoelekea iwapo hauna ramani ya kukuelekeza unapoelekea kuna wakati utapotea tu.Hakikisha unaweka maisha na mipango yako kwenye maindishi mara kwa mara ili kukusaidia kujiongezea hamasa ya kila siku kwenye maisha yako.Kumbukumbu zako hazitakudanganya na zitakusaidia kutambua makosa unayoyafanya na faida unazopata kutoka kwenye mipango ulio nayo kwenye maisha yako binafsi.

3. UWAJIBIKAJI HUONGEZEKA

Kwa namna ya kawaida kwenye maisha usipokuwa na kitu ambacho kinakujlisha kwamba unasonga mbele/unarudi nyuma mara nyingi unaweza kuishi maisha ya namna yoyote ile sababu hakuna kitu ambacho kinakuonyesha wala kukujulisha .Unapoweka maisha yako kwenye maandishi inakusaidia kutambua wapi unapaswa kuongeza juhudi za makusudi ili kuweza kufikia malengo mbali mbali uliojiwekea lakini unapokosa maandishi ni ngumu kutambua na kufahamu wapi unapaswa kuongeza juhudi na wapi unapaswa kupunguza vitu kadha wa kadha ili kuleta matokeo bora zaidi kwenye maisha yako na malengo yako ya kila siku ambayo umejiwekea.Muhimu kuhakikisha maisha yako yanakuwa kwenye maandishi mara kwa mara ili kuongeza ufanisi wako wa kiutendaji na uwajibikaji wenye tija kwako wewe binafsi.Epuka kuishi maisha yasiyo na uwajibikaji kwa kutokuweka maisha yako na mipango yako kwenye maandishi.

4. FAIDA KWA VIZAZI VIJAVYO

Unapofwatilia kw a ukaribu utagundua maisha yetu ya sasa ni sababu tunasoma kumbukumbu za kimaandishi za watu wengine ndio maana tupo hivyi leo tulivyo.Unaposoma vitabu mbali mbali vya dini/biashara/taaluma ,utagundua kwamba kumbukumbu zao zimekuwa muhimu kwetu binafsi zimeweza kutuvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine.Watu ambao wamekuwa wakifanya gunduzi mbali mbali kwenye maabara mpaka sasa tunafaidika na gunduzi hizo maana yake ni kwamba kila mara walipofanya majaribo waliweka kumbukumbu za kimaandishi nah ii imetusaida hata sisi kutambua kwamba wapi walikosea na wapi walipatia ili sisi tusirudia makosa yaleyale waliofanya wao .Kumbukumbu za kimaandishi husaidia kuongeza ubora wa kiutendaji kwa vizazi vijavyo na kuepusha kizazi husika kurudia rudia makosa yale yale kila siku nah ii kukutuanya kuishi kwa ufanisi na ubora zaidi.
E-mail: naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless You All.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.