HABARI PICHA: TAMASHA LA KUOMBEA AMANI TANZANIA LILIVYOFANA

Mama Salma Kikwete akiingia uwanjani pamoja na msafara wake.
Tamasha la kuombea amani Tanzania limetimia. Jumapili ya tarehe 4 Oktoba 2015, zikiwa zimesalia siku 20 kuingia chumba cha kufanya maamuzi juu ya kiongozi ajaye ndio siku ambapo tamasha hili limefanyika.

Maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake walijitokeza kwenye tamasha hilo ambapo mgeni rasmi Rais Jakaya Kikwete aliwakilishwa na mkewe, Mama Salma Kikwete. Upekee wa tamasha hilo umetokana na uwepo wa idadi kubwa ya waimbaji, ambapo kutoka Tanzania, Kenya, Nigeria, na hata Afrika Kusini zimewakilishwa, bila kusahau Zambia.

Gospel Kitaa ambayo imekuwepo mwanzo mwisho inakuletea picha za tukio hili lenye kutia hamasa ya umoja wetu na kulinda amani iliyopo, kama ambavyo limehudumiwa na waimbaji kutoka pande mbalimbali za dunia.

MGENI RASMIKinondoni Revival


Wakorintho Wa Pili Kutoka Iringa 

St. Andrew Anglikana Msalato Dodoma.


AIC Chang'ombe Choir CVC

Beatrice na Martha Mwaipaja


Christopher Mwahangila

Joshua MlelwaUpendo Kilahiro


Upendo NkoneBony Mwaitege
WAIMBAJI WAKIIMBA WIMBO WA AMANI KWA PAMOJASipho Makhabane (Big Fish)Solly Mahlanguwanamuziki wa Sipho wakifuatilia kile wanachofanya kundi la Solly


EMMANUEL MBASHA AKAAMUA KUPANDA JUKWAANI KUCHEZA NA PASROR SOLLY


Ifenye Kelech


Sarah K

Ephraim Sekeleti (Son of Tanzania)

John Lisu
Mkurugenzi wa Msama promotion akifurahi na mtoto wa John Lisu


Kwaya ya Uinjilisti - Kijitonyama KKKT

Rose Muhando

Ilipotimu mida ya saa nne usiku, Mwanamama Rose Muhando aliyeadimika masikioni na machoni mwa watu kwa mudamrefu sasa hatimaye akapanda kuhitimisha.Hili limetimia, tujiandae kwenda kupiga kura tarehe 25 Oktoba kwenye vituo tulivyojiandikisha, na kisha baada ya hapo tubaki kuhimizana kusubiri matokeo kwa amani bila shari ya aina yoyote ile.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.