HOJA: AINA ZA HAKI NA MATUMIZI YAKEAskofu Sylvester Gamanywa.
Mwangalizi Mkuu, WAPO Mission International.


Neno haki limechukua nafasi kubwa kwenye mijadala ya kampeni za kisiasa. Lakini pamoja na kutawala mijadala, bado kuna uelewa mdogo sawa kuhusu tafsiri sahihi kuhusu amani, aina za amani na matumizi yake. Na has katika eneo la msamiati wa “haki” inayotajwa kwenye Biblia na “haki” linalotumika katika jamii ya kawaida. Wengine wamechanganya wakifikiri haki inayotajwa ndani ya Biblia ndiyo haki hii hii inayotajwa katika mazingira ya kawaida ya kijamii. Mada hii nimeileta ili kuondoa utata uliopo:

Tafsiri ya aina za
haki na matumizi yake

Tafsiri ya jumla ya neno haki kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili limetafsirikuwa ni: (i) Jambo ambalo mtu anastahiki, au kitu anachostahili kuwa nacho. (i) Uendeshaji wa jambo kufuatia sharia au kanuni zilizowekwa.

Pamoja na tafsiri hii ya jumla, sina budi kukiri kwamba lugha yetu ya Kiswahili ni maskini kwa tafsiri ya maneno na hasa yanayotafsiriwa kutoka lugha za kigeni, hususan lugha ya Kiingereza.

Mathalan, msamiati wa neno “haki” kwa lugha ya Kigereza lina maneno yafuatayo: Justice and Righteousness. Japokuwa yote haya yametafsiriwa kwa Kiswahili kuwa ni “haki”; ukweli ni kwamba, hizi ni haki za aina mbili tofauti.

Neno “justice” lina maana ya “haki ya kisheria”. Na neno “Righteousness” lina maana ya “haki ya kimaadili”

Hebu sasa tuzifuatilie aina hizi mbili za haki kwa tafsiri za lugha asili kama ifuatavyo: Neno “haki ya kimaadili” kwa mujibu wa Biblia zimetumika lugha mbili tofauti ambazo ni kiebrania, na kiyunani. Haki kwa lugha ya kiebrania ni “tsaddiy” likimaanisha adili, halali, sahihi.

 Na lugha ya kiyunani ni “dikaios  likimaanisha “sheria za kiungu”, “unyofu”,” timilifu”, “kutokuwa na hatia,” “ kutokuhumika” Tafsiri zote hizi zinalenga sifa alizo nazo Mungu mwenyewe kuwa ni Mwenyehaki, Mnyofu, Mkamilifu.

Tofauti za mifumo zilizomo kati ya
haki ya kisheria na haki ya kimaadili

Baada ya kusoma tafsiri za misamiati ya aina mbili za haki, yaani “haki ya kisheria” na “haki ya kimaadili”; sasa tuchunguze tofauti zake za kimfumo:

Mfumo wa haki ya kisheria

Haki ya kisheria chimbuko lake ni Katiba pamoja na sharia za nchi. Na mfumo wa utoaji haki za kisheria unajulikana kupitia mihimili mkuu mitatu ya dola ambayo ni: Bunge, Mahakama, na Serikali za kiraia.

Mfumo wa haki ya kimaadili

Haki ya kimaadili chimbuko lake ni sharia, amri na maagizo ya Mungu katika kitabu kinachoitwa Biblia.


Kitabu hiki kina mkusanyiko wa vitabu ambavyo vimegawanyika sehemu kuu mbili. Kuna vitabu vya Agano la Kale ambavyo vinajulikana kwa jina maarufu kama vitabu vya Torati ambavyo ni sawa na “katiba” ya Mungu aliyowakabidhi taifa la Israeli iwaongoze. Huu unajulikana kuwa ni mfumo wa “utawala wa Mungu kwa binadamu” (Theocracy).

Kuna vitabu vya Agano Jipya ambavyo vinajumuisha Injili na nyaraka vyote vikitafsiriwa kuuwa ni “Neno la Kristo” kwa Kanisa la Agano Jipya.

Kabla ya kuhimisha kipengele hiki, napenda kusisitiza kwamba “Haki ya kisheria” inahusisha zaidi “Uhuru wa mawazo na maamuzi”, “fursa sawa kwa kila mtu na “huduma stahiki” kutolewa bila ubaguzi wala upendeleo.

Lakini “Haki ya Kimaadili” ni  uhuru wa kiimani unaozingatia utii kwa sharia za Mungu na kujenga mahusiano ya kiroho na Mungu. Tukichunguza uzito wa sharia ya torati na Neno la Kristo katika Agano Jipya, tunabaini kwamba, Torati ilikuwa ni katiba ya taifa la Israeli na kwa ajili ya wawa wa Israeli. Na sheria za Agano Jipya ni kwa ajili ya Kanisa pamoja na watu binafsi wanaoamua kumfuata Yesu Kristo wawe chini ya utawala wake kiroho.

Mapungufu yaliyomo kwenye
haki za kisheria na kimaadili


Sasa tunaingia kwenye eneo muhimu sana ambalo tunahitaji kulichambua. Nalo si jingine bali ni kuujua upungufu au udhaifu uliomo katika mifumo ya kisheria inayotakiwa kutoa haki stahiki.

  1. Upungufu uliomo katika “Haki ya kisheria”

Haki za kisheria si za kudumu milele, na huwa zinapitwa na wakati. Nasema hivi kwa sababu kutumia mfano wa karibu sana taifa letu Tanzania. Tangu tupate uhuru Katiba ya nchi imebadilishwa mara nyingi na hata hivi sasa bado kuna mchakato wa katiba mpya ambao umeahirishwa mpaka baada ya uchaguzi mkuu.

Kwa hiyo, ukifuatilia kwa makini utakuta kwamba, haki zinazopatikana kwa mujibu wa sheria zinaboreshwa au kudhoofishwa na aina ya sheria zilizopo kwa wakati uliopo.

  1. Sio kila sheria halali ni njema kimaadili

Japokuwa sheria zinazotungwa na vyombo husika zikiisha kupitishwa rasmi zinatambulika kuwa ni halali kwa matumizi. Ukweli unajulikana kimataifa kwamba si kila sheria halali ni sheria njema.

Ziko sheria nyingi ambazo zinatungwa kutokana na jamii kuingia kwenye matatizo ya kimaadili kwa ajili ya kujaribu kuhalalisha mambo ambayo hapo zamani hayakuwa yanakubalika kimaadili.

Nitoe mfano maarufu wa siku hizi kuhusu kampeni inayoendelea kimataifa ya kuhalalisha “sheria ya ndoa za jinsia moja.”

Udhaifu mwingine wa haki ya kisheria ni kuwepo kwa sheria nyingi zinazotungwa kwa madai ya kulinda haki za baadhi ya binadamu lakini zinavunja haki nyingine za binadamu  wengine katika jamii

  1. Upungufu wa sheria za haki ya kimaadili

Kwa asili sheria zote za Mungu zilizomo katika Biblia hazina upungufu hata kidogo. Tena tunasoma kwamba zinadumu milele. Yesu mwenyewe alithibitisha akisema kwa habari ya torati ya kwamba:

“Kwa maana amin, nawaambia, mpaka mbingu nan chi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” (Matt.5:18)

Na kwa habari ya maneno yake ambayo Yesu aliyasema katika kuthibitisha Agano Jipya nayo aliweka bayana kwa kusema kwamba:

“Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.” Lk.21:33)

Mbali na sheria za Mungu kuwa zinadumu milele, pia ni za kiulimwengu (universal). Zinatumika kila mahali bila kujali mipaka ya kijiografia,  bila kujali tofauti za rangi, kabila, jinsia, au tabaka. Kana kwamba hii haitoshi, Msimamizi wa sheria hizi ni Mungu mwenyewe na ndiyo maana hakuna binadamu yeyote mwenye mamlaka ya kubadilisha hata nukta moja

  1. Upungufu uko kwenye tafsiri na utekelezaji wake

Kushinikisha viwango vya sharia za torati kutaka ziwe mfumo wa sharia za kiraia/kijamii

Torati ilikuwa ni Katiba ya taifa la Israeli chini ya Utawala wa Mungu, ambapo wafalme, manabii na makuhani waliteuliwa na Mungu mwenyewe.

Itaendelea toleo lojalo
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.