JE UNATAKA KUMUONA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO?

Mtumishi King Sam


JE UNATAKA KUMUONA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO?
LAZIMA UWE NA ROHO YA KUHABUDU 

Kama unataka umuone Mungu na utendaji kazi wake lazima ukubali kubadilika toka kwenye desturi za ibada za dini,kuna watu wanamsisimuko wa kuhabudu Mungu siku za ibada Kama ni jumapili au Juma mosi au ibada ya katikati ya wiki,
Zaburi Psalms 95:6
Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

Yohane John 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Yoshua Joshua 24:14
Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.

MUNGU HANA SIKU YA KUMWABUDU, MUNGU NI ROHO NAYE ANAFANYA KAZI MASAA 24
Wewe nawe unatakiwa muda huo Roho ya kuhabudu inafanya kazi siyo siku flani ndiyo maana majaribu yanavyokuja yanawakumba wengi,kwa sababu wako kimwili zaidi,ngoja nikuambie shetani anajuwa kabisa akikukamata ni akupe ubize (busy) wa maisha ili akija ni raisi kukuzoa

Kanisa la Leo limekuwa dini na ndiyo maana unaona halina tofauti na dunia inaposema kanisa namaanisha wewe nikisama dunia namaanisha Mtu ambaye hajaokoka kwa hiyo jichunguze uone tofauti yako na yawale ambao hawajaokoka,Kama wanamatatizo ya magonjwa umasikini na kushindwa nk JE wewe unashida magonjwa? Biblia inasema sisi maana yake kanisa in Nuru ya ulimwengu JE wewe ni Nuru?

Ukichunguza ndani ya kanisa watu wengi wanamsisimko wa kuhabudu na si kwamba wana Roho ya KUHABUDU ndiyo maana akitoka kwenye msisimko matatizo shida ziko pale pale yeye anakuwa Mtu wa kawaida tabia zake zinarudi mpaka unashangaa hivi ni Mtu Yule au,badilikeni
Mwambie Mungu akupe Roho ya KUHABUDU aubadilishe moyo wako na kukupa moyo wa nyama moyo wa kunyenyekea mbele zake katika jina la Yesu,

Ezekieli Ezekiel 36:26
Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.

Kuna watu wanahabudu kwa mazoea hatuhabudu kwa mazoea bali kwa kuongozwa na Roho ndiyo maana Kama hauna Roho ya kuhabudu utakuwa Mtu wa mazoea na Mtu wa dini,unafikiri mpaka umekuwa kwenye kanisa ndipo unaibada ibada ni popote ulipo

Nini maana ya KUHABUDU? Wazungu wanasema Worship
Tutaona sehemu ya pili.....

Jumapili yangu ni Monday to Monday usiku na mchana namwabudu Mungu niwe kazini au ukitaka shetani akukamate uwe Mchungaji au mshirika uwe na desturi ya kwenda mbele za Mungu wakati unapojuwa kesho ni jumapili au jumatano au jumamosi siku ya ibada ndipo unajiandaa kwa Neno na kwa kufunga na mazoezi ya Nyimbo,nasema kwa jina la Yesu badilika

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.