KWA TAARIFA YAKO: RAIS ALIVYOIKABIDHI NCHI KWA MUNGU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Rais wa Zambia, Edgar Lungu. ©Open Zambia
Kati ya vitu ambavyo vinatazzmwa kama mfano wa kuigwa, ni tukio la Rais Edgar Lungu wa Zambia kutangaza siku maalumu ya kufunga na kuomba kwa ajil taifa hilo jirani wa Tanzania.

Tarehe 18 Oktoba, wiki moja kabla ya kufanya maamuzi kupitia kura zetu kwenye uchaguzi mkuu, ndio siku ambayo wao taifa la Zambia watakuwa wakifunga na kuomba, wakililia rehema za Mungu.

KWA TAARIFA YAKO baadhi ya mambo yatakayowekwa kwenye maombi ni pamoja na hali ya kiuchumi, heshima iliyopotea kwa wazee, hali kubwa ya kutoajiriwa na umasikini miongoni wma vijana, kushuka kwa thamani ya Kwacha (fedha yao).

Jambo hili limeubua gumzo miongoni mwa wananchi wa mataifa mengine, wengi wakionekana kusifia huku wengineo wakiliona kama tukio la ajabu. KWA TAARIFA YAKO, taifa la Zambia ni mojawapo ya nchi ambazo zinajitabaisha kama taifa la Kikristo.

Wazambia nao wana mapokeo tofauti tofauti, wengine wakifurahia kama ambavyo Rais Lungu alieleza kwamba misingi ya taifa hilo kama ilivyowekwa na mababu, ni katika kumuamini Mungu. KWA TAARIFA YAKO hali iko tofauti kwa mtu mmoja ambaye hakupenda kujitambulisha kwa maelezo ya usalama wake, ambapo aliwataka wananchi kumuombea Rais badala yake, kwa kuwa anaanimi katika ushirikina tofauti na anayotamka kwenye hadhara.

Aidha chanzo cha habari kinaeleza zaidi kwamba pindi tu ambapo Rais Lungu alipotwaa madaraka aliagiza sangoma kutoka taifa jirani ili waweze kumlinda asipate kufa kama wale waliomtangulia. Aidha haijafahamika mara moja lengo la taarifa hizi iwapo ni za kutoridhika na lengo la maombi, ama kama ni kweli.

wachezaji wa timu ya  taifa ya Zambia ikimuomba Mungu kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012 ambapo waliwaa taji hilo
Pamoja nayo, hatua hii imeonekana kwamba ni ya ujasiri mkubwa, ambapo ni aghalabu taifa kufunga na kuomba baada ya kupata mwongozo kutoka ikulu moja kwa moja, ambapo imezoeleka makanisa yakiongoza jahazi hilo.

Hiyo ndio KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.