KWA TAARIFA YAKO TAMTHILIA YA EMPIRE ILIVYOANZA KUWACHEFUA WAKRISTO MAREKANI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Lucious na familia yake ambayo ndiyo kinara cha tamthilia ya Empire©cinemablend
KWA TAARIFA YAKO leo hii ni kuwataarifu watazamaji wa moja ya tamthilia maarufu ya nchini Marekani inayoendelea kujizoelea umaarufu duniani iitwayo 'Empire' ambayo imeigizwa na nyota wa kuigiza wenye asili ya kiafrika. Kuhusu tamthilia hii ambayo imeanza kuonyeshwa msimu wa pili ama season 2 huku wiki hii ikiwa ni sehemu ya tatu, inadaiwa imejizoelea mamilioni ya watazamaji nchini Marekani inakoonyeshwa hususani waumini wa dini ya Kikristo.

KWA TAARIFA YAKO pamoja na kwamba tamthilia hii kujizoelea mashabiki wengi wakiwemo wa makanisani lakini tayari waandaaji wamejikuta matatizoni kiasi cha kudaiwa baadhi ya watazamaji kuanza kupungua baada ya kutajwa kwa jina la mwimbaji mkongwe wa injili duniani mchungaji Donnie McClurkin kwenye moja ya uigizaji ndani ya tamthilia hiyo kwamba nguli huyo atakuwa mmoja wa waimbaji watakaohudhuria kwenye tamasha la utolewaji tuzo za chama cha kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja kiitwacho LGBTQ kitendo ambacho kiliibua mjadala kwa waumini wengi kwa kutopendezwa na uamuzi wa waigizaji pamoja na watengenezaji kumtaja mwimbaji huyo kwenye jambo ambalo anapingana nalo.

Mchungaji Donnie McClurkin©CP
KWA TAARIFA YAKO jambo lingine ambalo linadaiwa limeanza kupunguza watazamaji hususani wa makanisani ni kitendo cha kuanza kujiita Mungu kwa mmoja wa waigizaji nyota wa tamthilia hiyo Terrence Howard ama Lucious jina la uigizaji ndani ya Empire kimewahudhi wengi kwakuwa hakileti picha nzuri licha ya kwamba ni uigizaji tu. KWA TAARIFA YAKO mchungaji McClurkin alitajwa na mwigizaji miss Lawrence ama anajulikana kwa jina la malkia wa mitindo ambapo alionekana amelala juu ya piano na kutaja jina la mwimbaji huyo kuhudhuria tuzo hizo jambo ambalo limemfanya mchungaji McClurkin kutoa ujumbe ambao ulipongezwa na wengi kwakuwa licha ya kutajwa jina lake kwenye jambo baya lakini ameamua kuwasamehe watengenezaji wa tamthilia hiyo tofauti na waimbaji wengine ambao tayari wameshafanya mipango ya kuwashitaki waandaaji wa tamthilia hiyo.

KWA TAARIFA YAKO mchungaji McClurkin katika kuweka mambo sawa moja ya maneno yake amesema alijua kutajwa kwake katika tamthilia hiyo baada ya kusoma jumbe kwenye mitandao yake ya kijamii kuhusiana na tamthilia hiyo inayoosheshwa na kituo maarufu cha FOX, amesema kitendo ambacho huenda kilipangwa kwa ubaya Mungu amebadili kwa wema, licha ya muongozo uliotumika na Lee Daniel mmoja wa watengenezaji wa tamthilia hiyo ambayo ni mwanaume anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja, imesaidia kuzua tahadhari kwenye injili ya Kristo Yesu ambayo ndiyo aimbayo, kuhubiri na kuwezesha, kisha nguli huyo aliwashukuru mashabiki wote wa injili ambao amewaita madada na kaka zake kwa ushirikiano wao, kumtia moyo na upendo walioonyesha kwake na kuwataka kutoonyesha ubaya kwa Lee Daniel zaidi ya kumuonyesha Upendo wa Kristo alisema mchungaji huyo.

Waigizaji nyota wa Empire Terrence na Taraji katika pozi©billiboard
KWA TAARIFA YAKO inadaiwa kitendo cha waandaaji hao kutaja jina la mchungaji huyo katika eneo ambalo lina utata ni kwasababu ya mchungaji Donnie McClurkin kupitia maisha hayo enzi za utoto wake pale alipobakwa na mjomba wake akiwa na miaka 8 kisha kutendwa jambo hilo tena na mtoto wa mjomba wake wakati akiwa na miaka 13. Mchungaji huyo aliweza kumjua Mungu lakini amesema badala ya watu wa kanisani kumsaidia kukaa karibu na Mungu na kuachana na tabia hiyo badala yake walimchukua na kumuunganisha na watu wanaojihusisha na vitendo hivyo na kujikuta huko lakini Mungu aliweza kumtoa katika tabia hiyo miaka michache baadae na hajarudia mambo hayo tena na huwa na kawaida ya kupinga mapenzi ya jinsia moja na kwamba watu wanaweza kubadilika na kuachana na tabia hizo wakimaanisha. Historia yake ya nyuma na tabia ya kukemea vitendo vichafu yawezekana ndio maana inadaiwa jina lake kutajwa kwenye sehemu hiyo.

Lee Daniels mtengenezaji wa Empire ©thesourceHiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo kama ulikuwa hujui, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.