MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUKUZUIA KUFIKIA KIWANGO CHA JUU CHA MAFANIKIO YAKO



Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.


1. TABIA YA KULALAMIKA

Moja ya tabia ambayo ni kikwazo kikubwa na kwa watu wengi kinachowafanya wasifikie kiwango chao cha juu cha kufanikiwa ni malalamiko.Mara nyingi kulalamika ni ishara ya kwamba una tabia ya uvivu na uzembe ambayo imejengeka ndani mwako.Kulalamika mara kwa mara huvuta nguvu hasi kwenye maisha yako ambayo hukufanya kuona kanakwamba kuna jambo ambalo haliwezekani kufikika kwenye maisha yako.Aina ya tabia ulio nayo ni mchango mkubwa sana kuelekea kufika mafanikio yako katika maisha ya kila siku.Tabia yako binafsi ni mtaji mkubwa sana kuelekea kilele cha mafanikio yako .Ni muhimu kuepuka kuwa na tabia ya kulalamikalamika maana inaonyesha ni namna gani ambavyo haujakomaa kiakili na kitabia kwenye maswala mbali mbali katika maisha yako ya kila siku.

2. VISINGIZIO

Iwapo unahitaji kufanikiwa kwenye maisha yako binafsi kwenye ngazi yeyote ile ni kuepuka visingizio visivyo na maana.Mara nyingi namna tabia na malezi yetu ya kitanzania tumejengwa kwenye maisha ya visingizio vingi na maneno mengi ambayo muda mwingine hayana tija kwenye maisha yetu ya kila siku.Hakuna mtu ambaye alifanikiwa kwenye jambo lolote muhimu kwenye maisha kwa kuweka visingizio vya mara kwa mara .Wazo la mtu ni mtaji tosha wa kuweza kukufanya ukafikia kiwango cha juu cha mafanikio kwenye maisha yako.Visingizio vingi ni ishara ya kwamba unakwepa majukumu yako na ni ishara ya kwamba hauko tayari kuweza kupika hatua mpya kwenye maisha yako ya kila siku kwenye jambo lolote.Jifunze kuepuka visingizio visivyokuwa na maana ,hakikisha unafanya na kutekeleza kwa ukaribu kile kitu ambacho unapaswa kukifanya kwa wakati husika mpaka kifikie tamati.

3. UOGA

Uoga wa jambo lolote lile huwa unaanzia kwanza kwenye akili ya mtu,hakuna kitu ambacho kinaweza kumtawala mtu bila kuingiza aina fulani ya uoga kwenye akili yake. Uoga ni neno rahisi sana kwenye maisha yetu ya kila siku na tumekuwa tukilitumia mara kwa mara lakini bila kujua aina ya athari iliyo nayo kwenye maisha yetu ya kila siku.Uoga wa kuogopa kujaribu kitu kipya au kufanya zaidi ya pale unapofikiria ni kikwazo kikubwa cha kukufanya usiweze kufikia mafanikio yako kwa urahisi na uharaka.Iwapo unatamani kwenda kwa kasi kubwa na yenye nguvu na isiyotetereka kwenye maisha yako ya kila siku adui wa kwanza unayepasa kumuondoa kwenye maisha yako ni UOGA.Hautaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote lile iwapo bado unasumbuliwa na kiwango cha juu cha uoga.Chukua hatua mpya na ujaribu kitu kipya bila uoga na ndipo unaweza kuona unapata hatua mpya kwenye maisha yako ya kila siku na ndipo unapoweza kuonja ladha ya juu ya kufanikiwa kwenye mambo mengi maishani mwako.

4. KUJIDHARAU/KUTOJIAMINI

Kutokujiamini katika kile ambacho unafanya ni ishara ya kwamba hatua za kufikia mafanikio ambayo unayatarajia ni ngumu na inaweza kuwa ndefu pasipo sababu za msingi.Msingi wa kwanza kwenye kila unalolifanya kwenye maisha yako ni kuhakikisha unajenga tabia ya kujiamini bila kutetereka au kuyumbishwa .Epuka kupenda kujilinganisha na wengine kwenye kila unachofanya maana kila mtu ana ndoto na lengo lake kwenye maisha unachopaswa ni kujenga uwezo wa kujifunza kutoka kwa namna walivyofanikiwa na sio kujifwananisha kwenye kile walichofanikiwa.Kila mtu aina yake ya ndoto na mfumo wake kwenye maisha ya kila siku kuweza kufikia mafanikio ambayo anayatarajia.Hakikisha unajenga tabia ya kujiamini mara kwa mara na sio kuwa na kiburi .Kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha kati ya kujiamini na kiburi,Unaweza kufikiri unajiamini kumbe una kiburi na Unaweza fikiri una kiburi kumbe ni kujiamini kwa kawaida tu.Ni muhimu kujua kiwango cha kujiamini kinaishia wapi na kiburi pia kinaanzia wapi. 

E-mail: naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.