PAPA AKUTANA KWA SIRI NA MCHUNGAJI ALIYEKATAA NDOA ZA MASHOGA NA KUMTAKA KUSIMAMA IMARA

Papa Francis na Mchungaji Kim Davis©boingboing
Mchungaji Kim Davis aliyepata umaarufu mkubwa nchini Marekani kwa msimamo wake wa kukataa kutoa hati ya ndoa kwa wapenzi wa jinsia moja amekutana na mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ambaye inadaiwa amemtaka mwanamke huyo kuendelea na msimamo wake huo.

Katika taarifa iliyotolewa na wakili wa mchungaji huyo amesema Kim Davis alikutana na Papa usiku
Rozari alitoa Papa kwa Kim na mumewe©LibertyCounsel
katika kikao cha siri wakati mkuu huyo alipokuwa ziarani nchini Marekani. Ambapo kwa mujibu wa wakili huyo amesema Papa amemtaka mteja wake kusimama imara. Kukutana kwa watumishi hao kulithibitishwa kupitia rozari za kusalia zinazotumiwa na kanisa katoliki ambazo inadaiwa Papa Francis alizitoa kama zawadi kwa mchungaji Kim Davis na mumewe, huku mchungaji Davis yeye alitoa rozari yake zawadi maalumu kwaajili ya wazazi wake ambao ni waumini wa Katoliki

Ambapo kwa mujibu wa taarifa hiyo inasema Papa Francis amesema kitendo cha mtu kuzuiwa kutenda mambo kwa mujibu wa dini yake ni kinyume za haki za binadamu, ujumbe ambao umetafsiriwa kama neno kwa watu wa jimbo la Kentucky anakotokea mchungaji huyo kwa vitendo vyao wanavyovifanya. Unaweza kusoma taarifa kamili kuhusu kikao chao kwa kubonyeza hapa 

Mchungaji Kim Davis alilala jela kwa siku tano kabla ya kuachiwa ikiwa hukumu kutoka kwa jaji wa mahakama ikiwa adhabu yake ya kukataa kuidhinisha cheti kwa wapenzi wa jinsia moja, ambapo kuachiwa kwake inadaiwa ni baada ya kuafikiana na mahakama kwamba hatowakataza wafanyakazi katika ofisi yake ya kanisa kutoa vyeti hivyo kwa wapenzi wa jinsia moja huku mchungaji huyo akiweka msimamo wakutowekwa jina lake kabisa kwa cheti chochote kinachohusisha ndoa ya watu wa jinsia moja.

Unaweza kusoma habari ya kwanza tuliyoandika kuhusu kuachiwa huru kwa mchungaji Davis kwa kubonyeza hapa
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.