SHANGWE ZA GK NI MWIMBAJI MWINGINE WA KWETU PAZURI AAGA UKAPERA


Kama tulivyokuwekea wiki iliyopita katika shangwe za GK namna ambavyo Mungu ameachilia baraka za ndoa katika kwaya maarufu ya Ambassadors of Christ ya kanisa la Sabato Remera lililopo Kigali nchini Rwanda (BONYEZA HAPA KAMA HUKUSOMA), basi mlango wa baraka bado haujafungwa kwao, maana mwimbaji wao mwingine mwanadada Josephine Mutoni alifunga ndoa na mpendwa wake mwanakaka Allan Kabayiza ambaye ni mwimbaji wa kwaya ya Friends of Jesus nayo ya nchini humo Rwanda.

Kama ilivyoada, waimbaji wa Ambassadors walikuwa bega kwa bega na mwimbaji mwenzao kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Tazama picha za tukio hilo kuanzia ndoa ya kimila mpaka ya kanisani.


Ambassadors wakiimba kwa furaha katika harusi hiyo©AOCC


Wakati huohuo waimbaji wengine wawili Gicari na Joseph ambao walikuwepo katika taarifa tuliyotoa wiki iliyopita, ni kwamba ile ilikuwa ndoa ya kimila, ndoa rasmi ya kanisani inatarajiwa kufanyika jumapili hii, yaani kesho.
NIMEKUPATA YESU


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.