SIKUKUU YA VIJANA ILIVYOADHIMISHWA T.A.G AZIMIO REVIVAL ARUSHA

Tarehe 4 Oktoba ilikuwa siku ya kihistoria kwa Tanzania Assembliues of God. Upekee wa siku hiyo unatokana na maadhimisho ya siku ya vijana ambayo hufanyika kila mwaka. T.A.G Azimio Revival Christian Church ni moja ya makanisa Jijini Arusha yaliyoadhimisha tukio hilo ambalo limeambatana na kumsifu Mungu, igizo, ngonjera, shukurani, mafundisho, na kila aina ya shangwe katika kulisifu Jina la BWANA Yesu.

Zifuatazo ni picha za tukio kama ambavyo GK imefanikiwa kukuletea Roho wa Bwana akitawalaa katika uwepo wake


Igizo

Kwaya

Mwenyekiti wa vijana akimlisha keki mchungaji kiongozi, Emanuel Munisi.Katibu wa vijana, Boniphace akimlisha keki mmoja wa wakinamama, Mama Caren
Mama mchungaji akitamka maneno ya baraka kwa vijana baada ya kutunukiwa zawadi.
Mchungaji Kiongozi, Emanuel Munisi, alishindwa kuzuia hisia zake na kuwa mwenye tabasamu muda wote
Sehemu ya vijana na waumini katika picha
Kanisa la Azimio Revival lipo Jijini Arusha, Kata ya Elerai, Mtaa wa Azimio. Unaweza kufika kanisani hapo kwa kushukia kituo cha Soseji, ambacho kiko mkabala na supermarket ya Mariam, karibu na Arusha Meat, iwe unatokea Ngara motni ama Mjini.

Ibada ya Jumapili huanza saa tatu na nusu, na Jumatatu ndio siku ya vijana, wakati Jumatano ni siku ya mafundisho ya Biblia kuanzia saa kumi na nusu jioni.
Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.