SOMO: ADUI NDIYE KAKUPANDISHA MLIMANI, LAKINI UTASHUKA KWA USHINDI

King Sam.

Shalom Wana wa Mungu aliye hai;

JE unajuwa Adui ndiye amesababisha wewe kuupanda huo Mlima unaopanda Leo katika maisha yako hiyo shida uliyonayo ni Mlima huo ugonjwa ni Mlima huo umasikini ni Mlima hata kwenye ndoa kwenye biashara au kazi Kama kuna mapito una pitia juwa in Mlima lakini Leo Mungu anataka ujuwe utashinda katika jina la Yesu
Haijalishi ni Mlima gani una panda utashinda katika jina la Yesu


Samueli 2 Samuel 15:30
Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda.
31 Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili.

Umekuwa unalia huku ukiupanda huo Mlima wengine in marafiki zenu wamesababisha uupapande huo Mlima lakini Yule Adui ambaye amefikiri kuwa wewe kuupanda huo Mlima ndiyo umeshindwa yeye ndiye atakayeshindwa kwa jina la Yesu,kuupanda kwako Mlima siyo kunamaanisha umeshindwa hapana kuna ushindi mbele yako katika jina la Yesu,japo kunawatu wana kuzomea wanakutukana kutokana na hali unayopitia ngoja nikuambie Leo hao hao wanaokuzomea ndiyo watakuja kunyenyekea mbele zako katika jina la Yesu,

Mlima Wowote katika maisha yako ni jaribu lakini katika Hilo jaribu kuna ushindi katika jina la Yesu wewe simama kwa Mungu maana ndiko kunaushindi katika jina la Yesu,
Mathayo Matthew 4:8
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,

Juu ya huo Mlima kunaushindi kwa sababu Mungu amekuchagua amekupaka mafuta yake matakatifu usiogope anasema
Isaya Isaiah 43:5 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;
6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.
7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya

Utakapo shuka kwenye Mlima utashanga kila kitu kufunguka kwa sababu una ushindi vile ambavyo hauna no kwa sababu unapanda Mlima iwe Nina kazi Biashara Ndoa au elimu au watoto muda tu utakaposhuka Mlima utashangaa jinsi una fanikiwa katika Jina la Yesu
Mathayo Matthew 8:1
Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.

Yesu amekuchagua wewe kwa sababu ya hiyo Biashara au Ndoa au huduma au kazi au kutuza hiyo familia usiogope wanaokucheka usiogope rafiki kuwa Adui utashinda katika jina la Yesu.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.