SOMO: JE UMEFANYA VYEMA KUKASIRIKA? -MCHUNGAJI KILIMAMchungaji :John Kilima

Yona4:1-3”Lakini jambo hili lilimchukiza sana yona naye akakasirika.Akamwomba bwana akasema,nakuomba,Ee BWANA;sivyo hivyo nilivyosema,hapo nilipokuwa katika nchi yangu?Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarashishi;kwa maana nalijuwa wewe ni Mungu mwenye neema,umejaa huruma,si mwepesi wa hasira,u mwingi wa rehema,nawe waghairi mabaya.Basi,sasa Ee BWANA,nakuomba,uniondolee uhai wangu;maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Kimsingi sauti zawatumishi wa mungu ni kinywa cha mungu duniani,kama mtu mwingine ametenda kwa kutokujuwa ndiyo maana injili ya Kristo lazima ihubiriwe dunia yote.Watu wa Ninawi walikuwa hawajapata kusikia neno la Mungu ndiomana wamekuwa wakitenda yasiyo wapasa. Unaweza ukamuhukumu mtu kwa kutenda maovu lakini Mungu ni mwingi wa rehema na fadhili hivyo husamehe
Hata kama zambi zingekuwa ni nyekundu kiasi gani yeye huzifanya kuwa nyeupe kama theluji Isaya1:18’’haya njoni na tusemezane asema bwana dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana zitakuwa nyeupe kama theluji,zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama sufu’’
Tabia yakuona watu wengine wanaokolewa,mtu anakasrika tabia hiyo ni ya nani?inatokana na nani?Mwanzo3:1- 20 ukisoma maandiko matakatifu katika kitabu chamwanzo hapa utaona shetani alipona mwanadamu ameinuliwa juu akatafuta kumwondoa katika utukufu na sifa mbele za mungu,shetani anaweza ingia ndani ya mtu ikiwa tu ameacha mlango wazi,sikuzote shetani hutafuta mwanadamu aaibike, baada ya Adamu na Eva kula yale matunda wakajikuta wamefunguliwa macho,ndipo Adamu na Eva wakajificha mbele za uso wa Bwana baada ya kuona wako uchi,walikubali kuaibika mbele za Mungu kwa kushindwa kumtii Mungu ndivyo tulivyo sisi kwa sababu si kweli tunatenda mambo yanayompendeza Mungu la hasha,mambo yetu yakawaida yasitutenge na Mungu wala kitu kiwacho chochote,macho ya Mungu yamejaa kuenea kote duniani ni vizuri kw a mwaminifu mbele za Mungu.
Jambo lakwanza tunagundua shetani ndie anae sababisha watu kukasirika,shetani alikuwa kerubi afunikae kwa uzuri. Isaya.14:13-
Yuda alikasirka wakati yesu alipo panda juu ya punda tusiwe kama Yuda kukasirikia wengine wanapofanikiwa,unapokasirika pale wengine wanapo inuliwa mwisho wako ni kutupwa pande za mwisho wa shimo,mtu ambaye alikasirika baada ya wengine kusamehwa 2Samweli13:1-13,15-16. Hapa utajifunza na kuona kwamba yeyote anayekasirika mtu anapofanikiwa basi ujuwe ndani kuna lusifa.
Kaini alimuuwa nduguye kwa sababu alipata mafanikio mbele za mungu mwanzo.4:1-
Mkuu wasinagogi alikasirika kwa sababu ya mwanamke kufunguliwa udhaifu wake siku ya sababu,wachawi hawapendi kuona mtu anafungulwa mafundo yao,wanachokifanya ni kumkosesha utulivu na kuanza kuona usumbufu kwa kile walicho kipata,na ukitaka kufanikiwa kuwapata watu waje kwa yesu ni lazima kuzibomoa madhabahu za mashetani,unapoanza kuinuliwa watu kutoka mbali huanza kukuaon kutokea mbali,kila unapoinuliwa wapo wanaokasirika,imeandikwa bwana ataninuwa juu ya watesi wangu,usiogope wala usifadhaike mimi niko pamoja nawe,tazama utawatafuta wala huta waona tena wala mahali pao hapata onekana tena.

Ufufuo na Uzima
Tanga

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.