SOMO: KANUNI ZA KUMSHAURI MFIWA ANAYEHUZUNIKA SIKU ZOTE

Mchungaji Peter Mitimingi, Mkurugenzi wa huduma ya Sauti ya Matumaini (VHM)
UMUHIMU WA USHAURI WA KIBIBLIA
1. Katika maisha tunahitaji Ushauri wa hekima (wise counseling) vinginevyo tutashindwa kuwa vile Mungu anavyotaka.
Mithali 15:22
22 Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.
2. Huduma ya Ushauri Huliponya Taifa na Kuleta Wokovu
Mithali 11:14
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
3. Ushauri unasaidia kupambana na mambo yasiyofaa na kuleta wokovu katika maisha ya mwanadamu
Mithali 24:6
6 Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
4. Yesu anatamulishwa kama Mshauri wa Ajabu
Isaya 9:6
6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
5. Yesu ametujaza Hekima na maarifa ya Kuwasaidia wanadamu kwa njia ya ushauri.
Wakolosai 2:3
3 ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.


6. Hekima na Ushauri Bora unatoka kwa Yeye Mungu
Ayubu 12:13
Hekima na amri zina yeye Mungu; Yeye anayo mashauri na fahamu
7. Ushauri unaleta njia ya kutokea
Mithali 1:5
Mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
8. Wanaotafuta ushauri, hupata amani na furaha
Mithali 12:20
Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.
9. Mshauri akitoa ushauri mbaya usiojenga afanya machukizo mbele za Bwana
Mithali 15:26
Mashauri mabaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maneno yapendezayo ni safi.

10. Ushauri unaleta mafundisho na hekima katika maisha ya mwanandamu
Mithali 19:20


BAADHI YA MAMBO AMBAYO HUWEZA KUSASABISHA HUZUNI (GRIEF) KWA WATU MBALIMBALI NI PAMOJA NA:
1. Mtu Kufiwa na mpendwa wake.
2. Kupata talaka
3. Kustaafu kazi na hasa bila ya maandalizi yoyote.
4. Kupata ajali na kupoteza baadhi ya viungo kama kukatwa mguu, Mikono nk.
5. Mtoto kukuaga anapokwenda shule ya mbali.
6. Unapohama kikazi au makazi na kuachana na jirani au ndugu au marafiki zako mliopendana au jirani yako anapohama na kukuacha.
7. Kupoteza nyumba au kitu cha thamani.
Kuunguliwa na nyumba
Nyumba kusombwa na mafuriko.
Nyumba kutaifishwa na Benki.
Nyumba kudhurumiwa na wana ndugu.
Mambo yote haya huweza kuleta huzuni majonzi na simanzi.
Pamoja na kwamba mambo yanayosababisha huzuni ni mengi, zaidi ya yote huzuni hujitokeza sana mtu anapokuwa amempoteza mpenzi wake au mpendwa wake wa karibu au mtu maarufu anapokufa.
Katika somo hili tutazungumzia zaidi tatizo la huzuni inayoletwa kwa kufiwa na mtu wa karibu na namna ya kukabiliana na changamoto hiyo kupitia huduma ya ushauri yaani (grief counseling).


HATUA 5 ZA HUZUNI (THE 5 STAGES OF GRIEF)

Kuna hatua tano za huzuni au majonzi (grief) ambazo mtu aliyepatwa na huzuni huzipitia.

Hatua 5 za Mwitikio wa Hisia za Mtu Mwenye Huzuni;

1. Kukana (Denial)
Ni hatua ya mtu aliyepoteza mpendwa wake kukataa kuupokea ukweli wala kukubaliana na hali halisi na kubakia kukana kwamba taarifa alizozisikia haziwezi kuwa za kweli hata kidogo na hawezi kuzipokea wala kuziamini.

2. kujadiliana/kushindana (Bargaining)
Hii ni hatua ya pili ya mtu aliyepoteza mpendwa wake kuwa na mawazo mawili kwamba huenda tarifa alizo zipokea zikawa za kweli wakati huo huo kwa upande wa pili hakubaliani na taarifa hizo kwahiyo anakuwa nusu nusu anakubali huku anakataa.

3. Hasira (Anger)
Hatua ya tatu ni mtu huyu anakuwa na hasira kali sana na maumivu makubwa ya moyo na kujiuliza maswali mengi kwa nini hali hiyo imempata yeye na sio mtu mwingine. Mtu huyo anaweza kumlaumu na kumkasilikia Mungu na mtu yeyote yule atakayehisi kwamba amehusika kwa namna moja au nyingine.

4. Kukata tamaa (Despair)
Baadaye mhusika anakuwa mtu aliyekata tamaa kabisa na kuona maisha hayataweza kwenda vizuri tena na kuona maisha yemepoteza radha na kamwe huenda yasirudi tena katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali.

5. Kukubali Matokeo (Acceptance)
Hatimaye hatua ya tano mhusika baada ya kupitia hatua zote nne nilizozitaja hapo juu, mhusika anafika katika hatua ya kukubaliana na matokeo kwamba sasa naamini kuwa mpendwa wangu kweli amefariki na sitoweza kumuona tena akiwa hai. Ni hatua mtu anakubali matokeo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.