SOMO: SABABU CHACHE ZINAZOTUFANYA TUHESHIMU WALIOTUTANGULIANa Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor

SABABU CHACHE ZINAZOTUFANYA TUHESHIMU WALIOTUTANGULIA

I. USHAURI WAO NI BORA.

“Wahenga walisema ukimwona Nyani Mzee Ujue Amekwepa Mishale Mingi” . Maisha tulio nayo ni mapambano ya kila siku yasiyo na mwisho ambayo yana matokeo mbali mbali. Wazee waliotutangulia ni watu muhimu sana wa kuwasikiliza maana wao wana ujuzi mkubwa katika hii dunia kwa sababu mbali mbali . Mara nyingi vijna wengi wanaokuwa wanakuwa na maisha ya nadhari vichwani mwao lakini wazee mara nyingi huwa wanajua hali halisi ya maisha ya kila siku yalivyo na kwamba ukifanya aina fulani ya jambo unaweza kupata aina fulani nay a matokeo na pia unaweza kufanikiwa au hapana.
Unapomwona mtu mzima aliyekutangulia kwenye hii dunia ni muhimu kumsikiliza maana unaweza kujifunza yaliyo mengi kupita yeye ambayo muda mwingine yanaweza yasiweko kwenye vitabu na unaweza usiwe umefundishwa darasani .Elimu ya Darasani na Kwenye Makaratasi ni tofauti sana na elimu halisi ya mitaani tunapoishi na changamoto tunazokutana nazo.Muhimu sana kujenga utaratibu na tabia ya kuwasikiliza waliokutangulia maana wanaweza kukusaidia kukuvusha eneo moja kwa haraka zaidi .

II. WATAKUOKOLEA MUDA WAKO BINAFSI

Muda ni moja ya rasilimali ambayo ikipotea hawezi kuirejesha na thamani yake ni kubwa zaidi. Hakuna mtu anaweza kujua thamani halisi ya muda mpaka muda utakapopea ndipo unaweza kugundua. Kitendo cha wewe kurudia rudia makosa waliyofanya waliokutangulia ni moja wapo ya namna ya kupoteza muda pasipokuwa na ulazima lakini unapokaa na watu ambao wamekutangulia na ambao wana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo ni rahisi kukueleza na kukusaidi kutambua gharama za makosa ambayo waliyafanya na ambayo wewe haupaswi kuyarudia kuyafanya. Kuna namna mbili za kujifunza kutoka kwa wengine , kwanza tunajifunza kutokana na makosa waliyoyafanya wao na pia tunajifunza kutokana na mafanikio waliyoyafikia katika kipindi cha uhai wao. Ni muhimu sana kukaa chini na kuwasikiliza kwa kile ambacho wanakueleza. “Mtu asiyewasikiliza Walimtangulia,Kuna Wakati atalia na Asiwepo Mtu Wa Kumfariji”

III. HUFUNGUA MILANGO MIPYA YA NAFASI.

Kila mmoja wetu anahitaji nafasi mpya kwenye maisha yetu kuweza kufikia ndoto za maisha yake ya kila siku lakini namna tunavyoweza kufikia nafasi hizo ni kwa njia tofauti tofauti. Unapopata wasaa wa kuwasikiliza waliokutangulia unapata wasaa wa kutengeneza nafasi mpya kwenye maisha yako ambayo hapo mwanzo usingeliweza kuipata .Nafasi ya kuwasikiliza waliokutangulia inakupa uwanda mpana wa kuendelea kujifunza lakini pia kuweza kuongeza ujuzi wa ziada ambao kwa hali ya kawaida ungeweza kutumia gharama kubwa y a kuweza kuupata.
Kusikiliza ni Moja ya Taalamu ngumu ambayo watu wengi hatunayo lakini kwa kuwasikiliza waliokutangulia kunaweza kukusaidia kuongeza ujuzi na uwezo wa taaluma yako ya kusikiliza ambayo pia itakuongezea nafasi ya ziada ya kupata nafasi nyingine bora zaidi za kuweza kujifunza na kuongeza ujuzi wa ziada.

IV. PICHA HALISI YA TABIA YAKO.

Moja ya Picha halisi ya tabia ya mtu ni namna anavyowaheshimu watu waliomtangulia kwenye hii sayari .Unapomuona mtu anakosa adabu na heshima kwa watu waliomtangulia ni picha ya tabia yake ya ndani namna alivyo.Heshimu yako kwa watu waliokutangulia inasaidia wengine kujua taswira yako ya ndani ambayo kwa hali ya kawaida tusiipate. Tabia ya Mtu ya Heshima inakupa picha halisia ya maisha na jamii inayomzunguka kwa ujumla.Unaweza ukakosa nafasi muhimu kwenye maisha yako sababu tu ulikosa heshima sehemu fulani kwa mtu aliyekutangulia. Picha ya Heshima tunayoiona inatupa mwangaza namna ambavyo unaweza ukawaheshi wengine hata ambao uko nao katika hatua ya kawaida ya masiha yako ya kila siku hapa duniani. E-mail: naki1419@gmail.com 
+255788454585 
God Bless You All.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.