WEEKEND WORSHIP NDANI YA CCC JUMAMOSI HII


Hii ni Ibada ya kusifu na kuabudu inayofanyika kila Jumamosi ya kwanza ya kila mwezi na asilimia 99% ya Hii ibada ni uimbaji unaomtukuza na kumwinua Mungu. Na hivyo Ibada hii ni kwa kila mtu wa dini, kabila na rangi yoyote ile.

Lengo kubwa la ibada hii ni kujenga ushirika na Mungu wetu. Yesu anatupenda sana na anapenda ukaribu na sisi.

City Christian Centre Upanga mkabala na Mzumbe ndipo ibada hii hufanyika kuanzia saa tisa mchana hadi saa moja usiku.

Kwa nini Jumamosi? Ndo swali linalofuata....Ni siku ambayo watu wengi wanakuwa huru makazini, mashuleni, vyuoni mwao na wanakuwa na mikakati ya kufanya mambo yao binafsi kama mitoko na kadhalika. Na hapo ndipo Mchungaji Samuel Mwangati alipopata maono ya ibada hii.

Njoo tujiweke tayari kwa ajili ya ibada ya Jumapili popote pale unaposali. Tukutane CCC kesho kuanzia saa tisa mchana. Hakuna kiingilio.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.