YALIYOJITOKEZA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI TANZANIA

Kwaya ya Mt. Andrew kutoka Anglikana Msalato, Dodoma kwenye tamasha la kuombea amani ya Tanzania 2015 Jijini Dar es Salaam. Bofya kwa picha zaidi
Kila mwaka Watanzania wamekuwa wakipata fursa ya kufaidika na matamasha ya kimataifa yanayoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions. Kati ya hayo kuna tamasha la krismasi, tamasha la pasaka, matamasha yahusuyo uzinduzi, na hata matamasha yanayoendana na matukio, mathalani tamasha la kuombea amani ya taifa.

Kati ya haya matamasha yote, kumekuwa na mapungufu ambayo yanajitokeza kwenye idara mbalimbali, lakini kwa kutazama tamasha la pasaka ambalo limefanyika mara ya mwisho katika uwanja wa taifa, ni hakika kuna mabadiliko kadha wa kadha yanayohitaji kuzungumziwa, hasa upande wa muziki.

John Lisu na timu yake kwenye tamasha la Krismasi mwaka 2013. Bofya hapa kwa picha zaidi
Vyombo ni sehemu muhimu sana ya tamasha lolote lile, ambapo huweza kubadili taswira nzima ya tamasha, na hata kupelekea kuchukiwa ama kufurahishwa na tamasha zima. Awamu hii, Msama Promotions imefanikiwa kumudu suala zima la vyombo. Na kwenye hilo tunafikisha pongezi zetu, maana hata wananchi waliofanikiwa kwenye tamasha hilo walikiri kushuhudia maboresho hayo.

Lakini katika yote, kumalizika kwa tamasha saa nne usiku imekuwa jambo ambalo halijafurahisha wengi. Uwepo wa waimbaji wengi ni jambo jema, lakini kama waimbaji wamesheheni kisha utaratibu mzuri wa uimbaji haukuwekwa, hilo hudororesha mpangilio wa tamasha. Ni suala ambalo waandaaji wanapaswa kulizingatia kwa awamu nyingine.

Sipho Makhabane kwenye tamasha la pasaka mwaka 2013
Ikiwa tamasha limeletwa kama sehemu ya ibada katika kumsifu na kumuabudu Mungu, ni sharti MC pia akaacha kukatisha wakati muimbaji bado anahudumu. Hilo huondoa uwepo wa Mungu na hata jambo ambalo Mungu alitaka kufikisha wa watu wake kupitia muimbaji husika. Waimbaji pia huwa na jambo la kuzungumza zaidi ya kuimba.

Upendo Nkone akimuombea mmoja wa waliojitokeza kwenye tamasha la pasaka 2014 Shinyanga. Bofya hapa kwa picha zaidi
Sehemu muhimu pia ya kutazamiwa ni upande wa hotuba zinazotolewa na wageni rasmi/waalikwa. Muda mwingine risala na hotuba huchukua muda mrefu sana na hivyo kuchosha watu waliojitokeza. Licha ya kwamba ni muhimu kwa risala na hotuba, maana hubeba maono na dhana nzima ya tamasha husika, lakini inapochukua muda zaidi hupoteza mvuto.

Ni hayo machache tu kwa sasa, ila pia unaweza kueleza namna ulivyoliona tamasha kwa ujumla kwa kuweka maoni yako hapo chini. Uwe na wakati mwema.a

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.