HABARI PICHA: NIGHT OF SEBENE ILIVYOFANYIKA KATIKA JIJI LA ARUSHA


Ijumaa ya tarehe 13.11.2015 ndo ilikua Siku yenyewe ya Night of Sebene pale EAGT Elerai kwa Mch. Marko Haule, iiyoandaliwa na Church Boy Church Girl ikishirikiana na kikundi cha waimbaji wa bendi ya Efra Musica.


Usiku huu ulihudhuriwa na vijana mbalimbali toka jiji la Arusha wakiwemo wanafunzi toka Chuo cha Uhasibu (IAA) na Arusha Technical Center (ATC).

Tukio hiyo ilipambwa na waimbaji mbalimbali wakiwemo Abednego and the Worshippers, Arise Worship Team, Word (Nelson and Joel), PCASF IAA, Arusha Mass Choir na Efra Musica.

Kulikua na vitu vingi vizuri vilivyowavutia na kuwafurahisha watu wengi kama vile Abednego and the Worshipers walipogeuza nyimbo za tenzi zilizoeleka kuimbwa taratibu kuwa sebene,pia namna Wor.d walivyoonyesha umahiri mkubwa wa kupiga drums.

 Efra Musica walinogesha usiku huo kwa namna walivyojipanga kuanzia mavazi hadi namna ya kupanda jukwaani kwa ajili ya kumpa Mungu utukufu kupitia sebene.

Pia usiku huo wa sebene alihudhurua mgombea ubunge wa jijini Arusha ndugu Philemon Olais Mollel (MONABAN) ambae pia alipata fursa ya kuzungumza na watu kuhusu kujitambua kwao.

Vile vile mshauri wa Churchboy Churchgirl alifundisha juu ya Upendo wa Mungu na pia alieleza yakuwa Mungu anatupenda kwa namna na jinsi tulivyo. Watu wote walio hudhuria walipata nafasi ya kucheza na kumsifu Mungu kwa kushirikiana waimbaji.

 Lengo kuu la usiku wa sebene  lilikuwa ni kuliinua jina la Mungu juu kwani biblia inasema "Tukimuinua Mungu juu anawavuta watu wengi waje kwakee.

Kama GK ilivyofika katika usiku wa sebene ungana nasi katika picha.

Abednego na The Worshpperz katika uimbaji


Barnabas Philip akiendesha tukio zima la usiku wa sebene

 Venither Chilambo Akiongee kuhusu ChurchBoy ChurchGirl
 Venither akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa ChurchBoy ChurchGirl

 Mgombea Ubunge ndg. Philemon Olais Mollel akizungumza na watu waliofika katika usiku wa Sebene


 Huyu ndio mtoto wake Philemon Olais Mollel ambaye ni Olais 

 Mchungaji Marko Haule akizungumza  Hawa ndio Wor.D hapa unakutana na vijana wawili ambao ni Joel Andrew pamoja na Nelson Mugarula katika umahiri wao wa kupiga Drums
 Watu kufurahi upigaji drum wa vijana hao wa Wor.D ambapo kirefu chake ni Worship With Drums

 Efraa Musica Wakiingia kuanza usiku wa sebene rasmi
 Arise Worship Team 

 Mshauri wa Churchboy Chuchgirl akiongelea juu ya upendo wa Mungu Jay Vomo


Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.