JE NENO KUSHINDWA LISINGEKUWEPO KWENYE KAMUSI UNGETUMIA NENO GANI MBADALA?

Faraja Mndeme,
GK Contributor.

Hakuna mtu ambaye hajawahi kutumia neno KUSHINDWA kwenye siku zote za maisha yake. Kuna wakati fulani na kwenye mazingira fulani ulitumia neno kushindwa kama sio kwa namna ya kuongea basi yawezekana kwa namna ya kutenda na kama sio kwa namna ya kutenda basi yamkini kwenye namna ya kufikiri. Je neno kushindwa ni halisi au ni namna ya ambavyo tumejitengenezea wenyewe?

Umeshawahi kujiuliza wewe binafsi iwapo usingekuwa unalifahamu neno kushindwa ungetumia neno gani mbadala kwenye maisha yako? Je neno kushindwa lina athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?Je neno kushindwa ni halisi au tafsiri na taswira tu na hoja tulizojijengea kwenye fahamu zetu kwamba kama haukufanikiwa jambo fulani ni kushindwa?
Maneno mengi ambayo wanadamu tumekuwa tunayatumia mara nyingi hayana uhalisia na vile vitu ambavyo vyenye maneno/majina hayo . Mfano kuna uhalisia gani kati ya Neno/Jina Meza na meza halisi tunazotumia kwenye maswala mbali mbali mfano Kulia Chakula n.k

Je unafikiria meza ingeitwa chupa na ukazaliwa ukakuta inaitwa chupa usingetumia? Unaweza ukaona kwa mfano halisi huu kidogo kwamba inawezekana neno/jina linaweza lisiwe na uhalisia na kile chenye jina. Majina ya vitu tunayoyaona leo ni watu walibuni au yalizaliwa tu kulingana na jamii ilivyokuwa inatoka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo. Unaweza kukuta tangu mwanzo maana halisi ya neno KUSHINDWA haikuwa hivi ilivyo leo lakini neno hilo kwa sasa lina nguvu labda kuliko ilivyokusudiwa tangu mwanzo. Je nani alikuambia kwamba jambo lisipofanikiwa ni kwamba moja kwa moja umeshindwa? Muda mwingine maisha yanaweza yakawa yanakupa mwelekeo mwingine ambao ni mzuri zaidi ambao hapo mwanzo hukuwahi kuufikiria. Ni Muhimu kujiuliza je neno kushindwa ni uhalisia na ni namna ya tafsiri za kufikrika tulizojitengenezea.
Namna ambavyo ubongo na maisha ya mwanadamu yalivyo tangu mwanzo wa uhai wetu ni hasi. Kwa hiyo tangu mwanzo tumezaliwa mpaka tunakua tumejikuta kwenye mazingira hasi na kila jambo tunalolifanya ni hasi. Kisaikolojia hapo ndipo inapotupelekea watu na jamii hujitengenezea maneno au tafsiri fulani ili kuweza kujiridhisha na kujifariji hata kama tafsiri hio sio halisi na haina mashiko. Kushindwa ni neno la kawaida sana na huenda halina uhaisia na ukweli kwenye maisha yetu ya kila siku bali ni namna ambayo tumekuzwa kwenye jamii zetu. Hii imetufanya kuyapa uhai maneno ambayo muda mwingine hayakuwa na uhai na ukiongeza na mazingira hasi tuliyokuzwa nayo basi ndio inakuwa kama umechanganya petroli na bidhaa za milipuko kwenye ghala moja.
Tafsiri nyingi za vitu tulizo nazo kwenye maisha yetu ya kila siku si sahihi sana kwa sababu ndizo tulizozikuta kwenye jamii na maisha yetu ya kila siku yapo kwenye jamii husika.Ni muhimu kutambua maneno mengine tunayokutana nayo kwenye maisha yetu yak la siku hayana uhalisia bali ni tafsiri mbaya ambazo tumezipa uhai sisi watumiaji.Je unafikiri tangu uzaliwe usingekutana na neno KUSHINDWA kungekuwa na neno gani lingine? Ni muhimu sana kutokubali kuchukua jambo na kulingiiza ndani ya moyo wako na akili yako kwamba ndivyo lilivyo. Je unapogundua chakula kina sumu utakula? Hapana. Ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kila siku kuna maneno ukiyaingiza ndani mwako ni sumu kwa afya ya maisha yako na ubongo wako na mwisho wa siku unaweza kukuta unashindwa jambo fulani si kama haliwezekani bali ni aina ya sumu uliyokula na baada ya muda fulani itaanza kudhihirisha madhara halisi kwenye maisha yako ya kila siku.

Ni muhimu sana kuwa na tafsiri halisi ya matukio tunayokutana nayo kwenye maisha yetu na sio tafsiri za jamii zinasemaje. Ukianza kuchunguza kwa ukaribu kuna tafsiri nyingi kwenye jamii haziendani na uhalisia wa mambo. Ni muhimu kuwa na chanzo sahihi cha tafsiri ya vitu kwenye maisha yetu ya kila siku kuepuka madhara kwenye afya za maisha yetu na akili zetu kwa ujumla.

Email :naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.