JE UJIO WA TB JOSHUA WA NIGERIA NI KULETA UPATANISHO AU UJUMBE KWA TANZANIA?

Watumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Facebook nchini Tanzania wamebaki njia panda na maswali bila majibu baada ya kuwasili kwa nabii maarufu barani Afrika kutoka nchini Nigeria TB Joshua ambaye ameonekana katika picha mbalimbali akiwa amepokelewa uwanja wa ndege na mheshimiwa John Magufuli, huku pia akitembelea Ikulu ambako alikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake Jakaya Mrisho Kikwete.

Mazungumzo ya wanamtandao hao yamezidi zaidi baada ya nabii huyo kuonekana akiwa na aliyekuwa mgombea wa tiketi ya Urais kupitia CHADEMA ikiwa chini ya mwamvuli wa  Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Mheshimiwa Edward Lowassa. Hadi sasa haijajulikana ujio wa nabii huyo huku mazungumzo ya watu wengi wakisema yupo nchini kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa awamu ya tano au yupo nchini kuleta mapatano baina ya Rais mteule John Magufuli na aliyekuwa mpinzani wake Edward Lowassa kutokana na mengi na tabiri nyingi kutolewa endapo mmoja wa wagombea hao atakaposhinda au shindwa ni kipi kitakachoipata Tanzania.

Gospel Kitaa bado haijajua nini hasa ujio wa nabii TB Joshua nchini ila tutaendelea kufuatilia kujua hasa ujio wa nabii huyo kisha tutakujulisha...

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.