JOYOUS CELEBRATION YAKAMATA KILA PEMBE KWENYE TUZO AFRIKA YA KUSINIUsiku wa kuamkia leo huko nchini Afrika ya kusini kumefanyika utolewaji wa tuzo maarufu za injili ziitwazo SABC Crown Gospel Awards na kushuhudia waimbaji waliopikwa na kundi la Joyous Celebration wakiibuka na tuzo sambamba na waanzilishi wa kundi hilo wakipokea tuzo za heshima kwa mchango wao katika muziki nchini Afrika ya kusini.

Katika tuzo hizo zilizofanyika Durban, waimbaji waliowahi kuwika na Joyous walikuwa katika vipengele mbalimbali katika kuwania tuzo hizo akiwemo mwanadada kipenzi cha mashabiki wa kundi hilo Mahalia Buchanan ameibuka na tuzo ya "Best Newcomer" kati ya tuzo tatu alizokuwa akiwania, Mchungaji machachari Agu Uchechukwu maarufu kama Pastor Uche ameibuka na tuzo ya "Best of Africa" huku waanzilishi na viongozi wakuu wa kundi la Joyous Pastor Jabu Hlongwane, Mthunzi Namba na Lindelani Mkhize wakiondoka na tuzo ya heshima "Lifetime achievement" 

Aidha licha ya washindi hao lakini pia alikuwepo mwanadada Tebello Sukwene ambaye naye alikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho ingawa hakupata tuzo., huku kundi maarufu la Worship House kutoka jimbo la Limpopo wakiondoka na tuzo moja. Lakini pia kijana anayesimamiwa na kampuni ya Koko music iliyochini ya waimbaji wa zamani wa Joyous Nqubeko na Ntokozo aitwaye Ayanda Ntanzi hakufanikiwa kuondoka na tuzo licha ya kufanya vizuri kwa album yake nchini humo.

Mahalia Buchanan

Pastor Uche akiwa na Lindelani Mkhize wa Joyous Celebration


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.