MAMBO MUHIMU YANAYOSAHAULIKA KUTATHMINIWA JUU YA MALENGO YA MWAKA TULIOJIWEKEA


Na Faraja Naftal Mndeme
GK Contributor.

I. UKUAJI BINAFSI KITABIA.

Tukiwa tunakaribia kuumaliza mwaka huu kila alijiwekea malengo mbali mbali ili kuweza kuyafikia.Malengo ambayo yanaweza kufanyiwa tathmini na kiwango cha kufikiwa malengo hayo ni yale yalioko kwenye maandishi na sio ya kufikirika.Muda mwingi tunapofanya tathmini yetu ya kufikia malengo ambayo tumekuwa tumeyafikia kwa mwaka husika mara nyingi tunaangalia tu kwa kiwango gani tumefanikiwa kufikia lengo hilo bila kuangali lengo hilo lina athari gani chanya kwenye maisha yetu binafsi.Malengo yoyote kwenye maisha yetu ambayo hayana mchango chanya wa katika ukuaji binafsi wa kitabia malengo hayo mara nyingi kufanikwa kwake ni kwa muda tu na huwa hayadumu.Hakikisha Ukuaji wa Mafanikio yako Binafsi Unaendana sambamba na Ukuaji wa tabia yako binafsi kwenye maeneo mbali mbali ya maisha.Ukiona Mafanikio yako ni zaidi ya Ukuaji wa Tabia yako Binafsi basi tambua mafanikio hayo hayatadumu bali yatakuwa ya kitambo kifupi tu.

II. UKUAJI KITAALUMA/KIUJUZI.

Ni Rahisi Sana kufurahia kwamba umefikia lengo fulani kwenye maisha yako lakini upnde mwingine kwenye taaluma yako unaduma au upo chini ya kiwango.Ni Muhimu kujiuliza athari za malengo ulionayo kwenye maisha yako kila muda fulani unapojitathmini.Hakikisha malengo ulionayo yanakwenda sambamba na ukuaji wa taaluma yako na kama sio taaluma yako basi angalau unaongeza aina fulani ya ujuzi kupita malengo ambayo umekuwa ukipiga hatua mara kwa mara. Unapokuwa kitaaluma au kuongeza aina fulani ya ujuzi basi tambua hali kadhalika thamani yako katika soko inapanda.Malengo yoyote ambayo hayana machango katika ukuaji wako wa kitaaluma na kiujuzi basi malengo hayo huenda yanachangia kukudimiza chini kitaaluma.Hakikisha unapofanya tathmini yako pia unaangalia na eneo la kitaaluma na kiujuzi limekuwa kwa kiasi gani na unapaswa kufanya kitu gani.

III. UKUAJI WAKO WA KIMAHUSIANO NA WATU WENGINE.

Hakuna mtu anayeweza kuishi peke yake kwa kujitegemea kila kitu,Kila mtu anamuhitaji mwingine ili kukamilisha jambo fulani kwenye maisha.Wanadamu wote tumeumbwa kuuishi kwa kutegemeana ingawa inawezekana isiwe moja kwa moja lakini bado kila mmoja ana muhitaji mwingine ili kufanya sayari yetu hii kuwa sehemu salama na nzuri ya kuishi. Moja ya Eneo Mara Nyingi ambalo huwa hatuliangalii wakati tunafanya tathmini ni eneo la mahusiano yetu na wengine. Unaweza kujikuta unafanikiwa kufikia malengo yaliyokusudiwa lakini unawapoteza watu wako wa karibu ikiwapo familia,ndugu jamaa na marafiki.Ni Muhimu kuhakikisha unakuwa na usawa katika yote maana unaweza kukuta unajenga upande wa pili huku unabomoa upande mwingine.Ni Muhimu kuhakikisha unatathmini kiwango cha ukuaji wako wa kimahusano na wengine.

IV. KASI YA UKUAJI .

Kasi ya Ukuaji kuelekea malngo yaliokusudiwa ni muhimu pia ifanyiwe tathmini,Unaweza kukuta tunashangilia kufikia malengo hayo kila mwisho wa mwaka lakini kumbe ulipaswa lengo malengo husika yawe yameisha miezi sita iliyopita.Matokeo yake unaweza kukuta unashingilia kuona yaliotimilika kumbe unashangilia hasara ya muda. Waafrika wengi hatuna tabia ya kufanya mambo kwa kuzingatia muda bali tunajua kwamba kesho ipo na inatusubiri.Mara nyingi huwa napenda kupendekeza kwamba linalowezekana leo lifanyike leo maana hakuna aliyeiona kesho.Kuna uwezekano kwamba ungelifanya leo lingewezekana lakini kesho likakushinda sababu unakuwa na mlundikano wa mabo mengi ambayo pia yanakusibiri wewe na rasilimali kubwa ni muda ambayo pindi inapopotea huwa haina urejesho tena.Hakikisha Unafanya tathmini ya muda na kasi ya ukuaji wako kufika malengo unayokusidia kila mwaka. E-mail: naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.