MWAKA WA NNE WA SAFARI YA MATAMASHA YA KUCHEKA TENA


💥Shalom!
Amani ya Mungu iwe nawe unaposoma na kuelewa Ujumbe huu!

👏Moyo wangu umejaa shukrani sana ninapofika wakati huu, Ninapofikia mwaka wa nne wa safari hii ambayo kikawaida haijakuwa rahisi sana ila Ni ya Uhakika!

👮Baba yangu aligundua nina kipaji ila hakuwahi kudhani kama kitakuwa "Major", aliniletea nyenzo nyingi za kunifunza ila hata mimi sikuwahi kujiona kama Nitatambulika kwa "carrier" ya Uchekeshaji na Ushereheshaji!
Pamoja na kufanya Shule ya Msingi na Sekondari kuzidi sana...nilikuwa napenda sana sanaa ila Nilikuwa Mkristo na sikuwa namuona mtu wa kumuiga huko!
Mtazamo wa wengi wakati huo hata sasa kwa wachache waliona ama wanaona Sanaa haiwezi kuwepo kanisani ingawa maigizo wanapenda na hata Filamu ya Yesu iko Majumbani kwao...na hiyo kwao sio sanaa ila ikija kwenye Uchekeshaji, Ngonjera na Maigizo inaonekana kama sio mahali pake!

🎌Mazingira yalinivunja moyo,ila sikuacha kufanya hivyo hivyo, sikuacha kufundisha wengine na sikuacha kujifunza...lakini hatimaye nikapata Ufunuo wa Ufahamu kuwa...nisiporasimisha haitakuja kuwa Rasmi...basi Novemba 2011 nikaamua kuanza Mfululizo maalum wa Matamasha ambayo nitaratibu mwenyewe na kuongoza mwenyewe na siyo kusubiri hisani ama mwaliko mahali!

🔋Na kwa hakika kwa Ugumu, kwa kulipa gharama kubwa, kwa machozi na Viwango bora, safari ikaanza...iliendelea kwa Ugumu mpaka angalau Tamasha la 5 ndio nikapumua...Haikuwa rahisi kwasababu:
A.Ilinibidi kuelezea hii ni nini kwa kina kila mahali,kwa vyombo vya habari na hata washika dau wengine🔊

B.Ilinibidi kushiriki kikamilifu katika kuandaa maana hata wana kamati walitembelea imani yangu🎍

C.Ilibidi kufundisha na kuwaongoza wengine wa kufanya nao📹

🚜...Yaani ilikuwa ni kazi ya kuchonga barabara katikati ya pori kubwa..maana upingamizi mkubwa ulikuwa unatokea huko huko kanisani kabla ya kunielewa, ila nilielewa tu...Hakuna Maono ambayo huanza kwa rahisi ama kukubalika haraka haraka tu!

"Ukiona unaanza safari ya maono ya Kimungu na hakuna ukinzani wowote njiani,basi uwe na hakika kuwa maono hayo yana asili ya yeye ama   mmeongozana naye"

📚Kupitia safari hii mpaka hapa nimejifunza vingi sana...nimewaona marafiki wa kweli...Nimejua gharama halisi ya maono...Nimepata hekima ya sio tu kuamua bali wapi na namna gani niamue...Nilifanya maamuzi magumu,nikaingia  gharama ya kuua Mtaji wa biashara ili maono yatimie na hata kujipata kwa madeni...ambayo ilinichukua muda kulipa na kurejesha Mtaji ila yote katika yote...mwaka wa kwanza huo...Tukaouna wa pili huo...mara wa tatu huo na Sasa ni mwaka wa nne huo!🎻

🌺Nilianza nikiwa "single" na sasa Ninaye msaidizi! Na Richard pia na mwaka huu Mrema pia!
Na kwahakika wasaidizi wamekuwa wasaidizi kwelikweli!

🎒Ninajivunia na kuwashukuru sana sana watu wote walioanza nami katika safari hii kwa namna yeyote ile,siwezi kuwataja kwa Majina ila kwa hakika kila mmoja yuko moyoni mwangu...Zaidi kamati yangubya maandalizi inayokuwa na kuboreka kila leo na mwisho ila sio kwa Umuhimu ni wanafamilia wangu...Richard Chidundo "Baba Generous" ambaye tulianza naye tangu mwaka wa kwanza; Gerald Mrema; na sasa Princes Glory ambaye ndio mpya kabisa,Frank,Masai pamoja na wengine ambao siwezi wataja wote!

4⃣Namba nne ni kwetu imekuwa ni ya tafakari,shukrani na sherehe hasa tunapojiandaa kuanza mwaka wa tano wenye viwango vya juu zaidi vya maono haya!

🔮Mwakani tunautarajia kuwa mwaka Kujenga msingi kwa Maono makubwa zaidi...tunatarajia kufanya "Workshop" maalum za mafunzo,ukocha na Ushauri wa Vipaji katika Majiji ya Dar,Arusha,Mbeya,Mwanza na Mkoa wa Dodoma!

🎎Tunatazamia familia yetu kukua na kufikia Wachekeshaji, Wanamashairi,Wanangonjera na Waigizaji 100-200 watakaomaanisha na madhabahu ya Bwana kwa mwakani!

📝Ninawashukuru sana wana habari na wadau wote wa Sanaa za Kikristo Tanzania kwa kila mchango, nimekuwa narekodi nyimbo mara moja moja na zingine huwa naimba madhabahuni moja kwa moja na Kipindi hiki upo Wimbo wa Shukrani uitwao "HALELUYA" utapatikana tu mtandaoni!

💝Basi kwa pamoja niwakaribishe Jumapili ya Novemba 22,2015 ndani ya Hema ya VCCT (Victory Christian Centre Tabernacle), Mbezi beach A kuanzia saa tisa...ili tusherekee,Tucheke na tule keki tunapomshukuru Mungu na kuomba Neema ya kuendelea mbele zaidi!

🎤Mimi mwenyewe(King Chavala) nitakuwepo pamoja na familia yangu nzima sambamba na Samuel Yona, The Jordan Band pamoja na watu kadhaa wenye vipaji vyao watakaokuja kutuonyesha..yamkini na wewe unacho...Karibu sana!

📯Kutakuwa na mazungumzo maalum na Mchungaji Huruma Nkone na Muziki utashangizwa na DJ Moses toka Kiango Media!

🚀Ni kwa Neema tu, timefika hapa...watu walisema hatutafika popote na kuna wakati kibinadamu tulitaka kutekwa na fikra hizo,lakini Bwana ni mwaminifu sana na Ona sasa tumefika mwaka wa nne kwa salama!

💒Msisitizo wangu utabaki palepale...sanaa ya kawaida hufanyika Jukwaani ila inakuja agenda ya Ufalme wa Mungu...sisi hatufanyi jukwaani bali tunahudumu madhabahuni!

✨Mungu akubariki kwa Mchango wako wa hali na mali,maombi pamoja na kuwafikishia taarifa wengine,zaidi kufika Tamashani!
Ukiwa na swali,mchango ama jambo lolote waweza kunifikia kwa mawasiliano hapo chini!

😂😂😂LAUGH AGAIN CONCERT... 
Laugh,  Relax and Release Yourself in Christ!!!

Wako;
👑Mwasisi na Mfalme wa Ucheshi wa Kikristo Tanzania 
👒King Chavvah (MC)
+255 713 883 797
(Whatsapp/Call/Sim banking)
Instagram @kingchavvah
Twitter @kingchavala
E-mail: lacs.project@gmail.com

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.