SOMO: UNAONA NINI? JIFUNZE KUTHAMINI WATU

Elie Chansa
GK Staff Writer.

Mara nyingi ni rahisi sana kuhukumu mtu kutokana na vile tumuonavyo, wala hatuna haja ya kumsikiliza, kwani kwa kumtazama tu tunaweza dhani tumeshaijua maisha yake yote na kutoa hukumu kwamba huyu yuko hivi na hivi. Angetokea katuni huyu na kukuuliza unamuonaje, huenda ungeanza kumjibu kwamba "nakuona u hafifu, huna afya, umechoka" na kadha wa kadha.

Wamuonaje mtu huyu ©The Blazing Center
Lakini kupitia video ifuatayo ambayo imetenegenzwa kwa minajili kuonesha thamani ya kila mmoja wetu, twatumai utabadili mtazamo wako namna unavyowachukulia binadamu wenzako. Haijalishi mtu yu mzee kiasi gani ama ni mtoto kiasi gani. Bado kila mmoja wetu ana lengo la kutimiza hapa duniani.

Wazee wafuatao kwenye hii video wanaonekana wamejichokea (taswira ya kwanza), lakini mara baada ya kueleza walichofanya tofauti  inaanza kuonekana ndani yao, na kwamba wamefanya mambo makubwa kuliko hatanamna walivyochukuliwa mwanzo.


Hivi ndivyo ambavyo yatufaa kumchukulia kila mmoja wetu bila kumdharau. Unaweza kumtukana mtu mtaani na ukadhani wewe ndiwe wa thamani, kumbe kile unachofanya, na hata pesa ulizo nazo kuna mtu ameshawahi kufanya na kuwa nazo. Umtazamapo mtu, usimuone kama takataka, bali binadamu mwenzako mwenye thamani sawa na yako.

Video hii inakumbusha habari ya bwana mmoja ambaye amewahi kulazwa hospitalini kwa kipindi cha zaidi ya miaka  kumi akiwa amepoteza fahamu. Lakini kitu ambacho hakuna aliyejua ni kwamba alikuwa anaelewa kila kinachoendelea pale hospitalini, yani kwamba kila aliyemtembelea, maneno waliyokuwa wanaongea, na hata mama yake ambaye kuna muda alikata tamaa hata kuomba mwanae afariki ili maumivu yapungue. Alipokuja kupona na kuamka, alieleza hali hiyo. Na mwisho wa siku akasema, "Treat everyone with compassion and respect regardless of if you think they will understand or not." Yaani kwamba "mjali kila mtu kwa huruma na heshima bila kujali kama anakuelewa ama la".

Uwe na Jumapili njema.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.