ANGALIA JOYOUS CELEBRATION 20 ILIVYOREKODIWA

Siku ya jumamosi iliyoisha historia iliandikwa nchini Afrika ya kusini baada ya kundi maarufu la injili la Joyous Celebration kutimiza miaka 20 ya huduma kwa kufanya recording kubwa kuwahi kufanywa na kundi lolote la muziki wa injili ama duniani nchini humo ama kwingineko barani Afrika.

Tokio hilo embalo lilifanyika katika uwanja wa Moses Mabhida ulipo jijini Durban nchini humo. Ambapo kwa mara ya kwanza kundi hilo lilirekodi jumla ya nyimbo 75 kwa kupanda jukwaani mara tatu ikiwa tofauti wakati wa sherehe za miaka 15 ambapo walirekodi nyimbo takribani 50. Sherehe hizo zilipambwa na waimbaji waliounda kundi hilo enzi hizo pamoja na waimbaji wapya.

 Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopigwa na GK kama ujuavyo, tovuti yako ilihudhuria tukio hilo muhimu la kihsitoria ingawa hairuhusiwi kuingia na camera zenye viwango vikubwa kwenye maonyesho ya kundi hilo GK tulijitahidi kupata picha hizi kwa camera zetu ndogo maana kubwa zake ilibidi tuziache hotelini.

Joyous Celebration the 20th recording
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.