ASKOFU GWAJIMA KUZINDUA KITABU CHAKE CHA 20 KATIKA MKESHA MKUBWA HII LEO


Askofu mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima nchini Dkt Josephat Gwajima, anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya waumini wa kanisa hilo katika ibada kubwa ya mkesha wa kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016 katika kanisa hilo lililopo maeneo ya Ubungo jijini Dar es salaam.

Licha ya kipindi kirefu cha kusifu na kuabudu pia Askofu Gwajima anatarajiwa kuzindua kitabu chake cha 20 kiitwacho 'Mkate wa Kila siku' alichokiandika. Pia ibada hiyo itakuwa na vipindi mbalimbali vikiwemo vya neno bila kusahau maombi ya shukrani na kufunguliwa.


VITABU VILIVYOANDIKWA NA BISHOP DR JOSEPHAT GWAJIMA

1. Maombi ya Kushindana

2. Kanuni kuu za Kujenga Kanisa la Maelfu

3. Msingi wa Kiroho

4. Vifungo vya Rohoni, Mwilini na Nafsini

5. Hatari ya Ndoto

6. Ushindi kwa Damu ya Yesu

7. Maombi ya Kubomoa Madhabahu

8. Sheria 2 za Rohoni

9. Damu Inenayo Mema

10. Nguvu ya Msalaba

11. Mimi sio kama Wale

12. Fumbo la Mauti

13. Usingizi wa Kichawi

14. Michoro ya Giza

15. Baraka Katikati ya Mapambano

16. Vikao vya Uharibifu

17. Mashetani Katikati ya Uzao wa Wanadamu

18. Jinsi ya Kutunza Muujiza Wako

19. Kibali Kilichoibiwa Kutokana na Mume au Mke wa Kiroho

20. Mkate wa Kila Siku


Wasiliana nasi kwa namba 0717 727206 na 0718104333
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.