HIVI UNAPOKWENDA KANISANI UWA UNAKWENDA KUONA NINI?HIVI UNAPOKWENDA KANISANI UWA UNAKWENDA KUONA NINI?

Ujumbe kutoka kwa King Sam


Luka Luke 7:25
Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokula raha, wamo katika majumba ya kifalme.
26 Lakini, mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na aliye zaidi ya nabii.


KILE UNACHO KWENDAGA KUKIONA NDIYO KIMEKUFANYA UWE HIVYO KILA SIKU KILA WIKI KILA MIEZI NA KILA MIAKA UPO ULIVYO,

WATU WENGI UWA WANAKWENDA KANISANI KUONA MHUBIRI NA NDIYO MAANA HUYO MHUBIRI AKISAFIRI NA YEYE HAJI KANISANI,WENGINE NI KWA SABABU YA KIPINDI CHA SIFA MAANA KINASISIMUA KWA SABABU NIMGONJWA KWA SABABU ANAITAJI MAOMBI KWA SABABU ANATAKA BIASHARA KWA SABABU ANATAFUTA WACHUMBA KWA SABABU ANATAKA MTOTO NK

WACHUNGAJI WENGINE UTAKA KUTUMIA KULETA WAIMBAJI WENYE MAJINA ILI WATU WAWEZE KUJA KANISANI KWA WINGI LAKINI WANAOKUJA HUKO KANISANI SI KWA SABABU YA YESU NI KWA SABABU YA MWIMBAJI FULANI ANAYEKUJA HAPO,

MPAKA UMEMUONA YESU VINGINEVYO UTAWEZA BAKI NA SHIDA YAKO MPAKA MWISHO
Yohane John 5:6
Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.

KUNA WAKATI YESU YUPO HAPO KANISANI LAKINI KWA SABABU WATU HAWAENDI KUMTAFUTA ILI WAMUONE NDIYO MAANA WANATOKA WALIVYO HAKUNA MTU ALIYEMUONA YESU AKABAKI ALIVYO HAKUNA TAFUTA KUMUONA YESU NAWE UTAMUONA KATIKA JINA LA YESU,

ANGALIA ZAKARIA ALIKUWA NA DESTURI KAMA YA KWAKO ULIYO NAYO UNAPOKWENDA KANISANI ALIKUWA HANA MTOTO MIAKA MINGI SANA LAKINI SIKU ALIPOMUONA YESU ALIPOKEA BARAKA ALIYOKUWA HANA MIAKA MINGI
Luka Luke 1:9
kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.
10 Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba.
11 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.
12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.

HACHENI DESTURI ZA KWENDA KANISANI KWA SABABU YA MAISHA NENDA KANISANI KUMUONA YESU NA TABIA HII YA KUWA DESTURI YA KUMTAFUTA YESU NI SIKU YA JUMAPILI UTASUBIRI SANA MAISHA YAKO KUBADILIKA MIMI SINA TABIA YA KUKUTABIRIA WAKATI HAUNA USHIRIKA NA MUNGU NDIYO MAANA TUNAONA KAMA MUNGU HAJIBU MAOMBI KUMBE MUNGU ANAJIBU HATA KABLA HAUJAOMBA WEWE ULIYE NA USHIRIKA NAYE
Isaya Isaiah 65:24
Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.

BADILIKA KWANZIA LEO ILI NA MAISHA YAKO YABADILIKE UNAPO KWENDA KANISANI USIENDE KAMA DESTURI YA DINI KWA SABABU NI SIKU YA IBADA BASI UNAKWENDA,NENDA KWA SABABU UNATAKA KUMUONA YESU ILI MBADILISHA ULIVYONAVYO NA WEWE UCHUKUWE ALIVYO NAVYO,
SHALOM
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.