HOJA: NINI MAANA YA KUMALIZA MWAKA

Askofu Sylvester Gamanywa
WAPO Mission International.


Kila mwisho wa mwaka kumekuwepo utamaduni wa kuadhimisha kile kinachoitwa kumaliza mwaka na maadhimisho ya kuanza mwaka mpya. Katika salamu zangu za kumaliza mwaka napenda tutafakari hasa ni nini maana ya kumaliza mwaka.

 
Vitu ambavyo havina
maana ya kumaliza mwaka

Kumaliza mwaka sio tu kubadilisha namba ya mwaka toka 2015 kwenda 2016. Kubadilisha namba hakuleti mabadiliko yoyote zaidi ya kubadili namba tu.

Na wala kumaliza mwaka hakuna maana ya kubadilika kwa mazingira toka kwenye uchakavu kwenda kwenye upya. Wala kubadili mwaka sio kuondoa changamoto za maisha ulizokuwa nazo na kuingia kwenye maisha raha bila masumbufu yoyote ya maisha.

Kimsingi, kumaliza mwaka kwa maneno tu kwamba tumemaliza mwaka hakuna mabadiliko yoyote yenyewe kuhusiana na mabadiliko ya mwaka. Tena unaweza kushangaa kwamba, unamaliza mwaka ukiwa katika hali nzuri na unapoanza mwaka mpya unauanza kwa mabalaa na majanga utadhani ni mwaka ndio una nuksi.

Kama haya yote hayana maana ya kumaliza mwaka, je ni kwanini suala la kumaliza mwaka linagusa sana hisia za watu wengi kila mahali duniani? Kwanini kumaliza mwaka kunasherehekewa kana kwamba kuna kitu watu wanapata wanaposherehekea? Kusema kweli ziko sababu mbali mbali zinazowasukuma watu kutoa uzito kwa sualala kumaliza mwaka nitazitajaa baadhi hapa chini.

Uzito wa kumaliza mwaka
uko kwenye sababu za kiibada

Ushahidi wa kihistoria unaonesha kwamba suala zima la kuadhimisha kumaliza mwaka na kuanza mwaka mpya zimebeba uzito wa shughuli za kiibada iwe kwa Mungu wa kweli au miungu/mizimu ya ukoo. Ndiyo maana waabudu mashetani/mizimu lazima waende makwao kutambika.

Kundi la watu waabuduo mashetani na mizimu wanapomaliza mwaka ibada zao kwa mashetani pasipo wao kujua huwapunguzia umri wa kuishi na kujiweka tayari kwa maisha ya nuksi na laana ya maisha ya kipindi cha miezi 12 ya mwaka unaofuata.

“..Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, tazama ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi” (MH.1:9)

Kwa kadri mtu asiyemcha Mungu anavyozidi kuishi duniani mwelekeo wake ni kumaliza vibaya na kuishi kwenye uangamivu wa kutisha kwa sababu ya maisha ya uovu aliyotumikia akiwa hai duniani:“Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; na matumaini yake huyo mbaya huangamia.” (Ayb.8:13)

Kumaliza mwaka pamoja na
Mungu huzalisha jambo jipya

Kama tulivyokwisha kupitia hapo juu ya kwamba, kutokumcha Mungu kunazalisha balaa zaidi, na hakuna jambo jipya kwa wasiomcha Mungu! Sasa tunapokuja kwenye kundi la wachaji Mungu mambo ni tofauti kabisa. Hapa tofauti tena haiko tu kwenye kumaliza mwaka mmoja na kuingia katika mwaka mwingine; bali ni jinsi tunavyomaliza mwaka tukiwa na mahusiano chanya na Mungu kiimani.

Hii ni kwa sababu Mungu mwenyewe ndiye mwenye kufanya jambo jipya kwa hao wamchao ili kudhihirisha kwamba wao pia ni watu tofauti chini ya jua. “Tazama nitatenda eno jipya; sasa litachipuka; je hamtalijua sasa?             Nitafanya njia hata    jangwani, na mito ya maji nyikani.” (Isa.43:19)

Kimsingi, kwa wachaji Mungu kwao kumaliza mwaka ni kufikia kilele cha utumishi kwa Mungu na wanawajibika kufanya ibada kwa fursa waliyopewa na Mungu kumtukuza katika maisha mafupi hapa duniani. Na wanapofanya ibada ya shukrani ya kumaliza mwaka wanajiweka wakfu kwa fursa nyingine ya kipindi cha miezi 12 ya utumishi mpya.“Tazama nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.” (Isa.43:19)

Mwisho wake mchaji Mungu ni tofauti kabisa. Maandiko yanasimulia kwamba, Mungu anamuwazia amani na tumaini afikiapo mwisho wa kuwepo kwake duniani.“Ninajua mawazo ninayo wawazia ninyi, asema BWANA ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” (29:11)

mwisho
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.