KWETU PAZURI WAZINDUA DVD MPYA YA 12 KWA KISHINDO JIJINI KIGALIKwa wale wapenzi wa kwaya iliyojizolea umaarufu Afrika mashariki na kati bila kusahau baadhi ya nchi kusini mwa Afrika ya Ambassadors of Christ kutoka Rwanda wiki iliyopita kwaya hiyo ilizindua DVD yake ya 12 katika tamasha kubwa lililohudhuriwa na maelfu ya waumini wa kanisa Sabato na makanisa mengine kutoka nchini humo na nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania.

Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya ukumbi wa Gikondo Expo uliopo jijini Kigali nchini Rwanda huku jina la album hiyo ikijulikana kama 'Hejuru Mukirere', uzinduzi ambao pia ulishirikisha vikundi mbalimbali ikiwemo kwaya ya vijana ambayo ilianzishwa na Ambassadors ama unaweza kuwaita Ambassadors B.Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.