MISS MAREKANI AMBWAGA MPENZI WAKE BAADA YA KUKATALIWA MAPENZI KABLA YA NDOA

Tim Tebow na mrembo Olivia Culpo

Katika hali isiyo ya kawaida au kuzoeleka katika bara Afrika huku bara la Ulaya au Amerika ya kaskazini kuwa kitu cha kawaida. Msichana mrembo ambaye amewahi kuwa Miss USA pamoja na Miss Universe aitwaye Olivia Culpo ametangaza kuachana na mpenzi wake mcheza mpira maarufu wa Marekani aliyeokoka Tim Tebow baada ya kijana huyo kuonyesha msimamo wa kutofanya mapenzi na mrembo huyo kabla ya ndoa.

Wapenzi hao walianza uhusiano mwezi Octoba mwaka huu huku mlimbwende huyo anayesifika kuwa na urembo wa kumshawishi mwanaume yeyote kushawishika kulala naye, hakujua kwamba suala hilo lingekuwa gumu kutokea kwa mwanamichezo huyo. Ambapo tangu msichana huyo kutangaza uamuzi wake umepokelewa kwa hisia tofauti na watu ambao wengine wameonekana kumponda Tim wakisema labda ni shoga kutokana na msimamo wake huku wengine wakimpongeza hasa kwa msimamo huo ambao ni nadra kupatikana kwa wanaume au wanawake wa sasa wakutoshiriki tendo la ndoa kabla tukio husika.


Olivia Culpo
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kama ilivyoripotiwa na gazeti la New York Daily News amesema, mwanamichezo huyo alikuwa amempenda msichana huyo sambamba na kumtumia jumbe mbalimbali, barua za mapenzi kumuonyesha mapenzi msichana huyo lakini ikawa ngumu kwa mrembo huyo kwani ameshindwa kustahimili katika uhusiano wao wa kutoshiriki tendo mpaka baada ya ndoa.

Mlimbwende huyo ameshakuwa kwenye mahusiano kabla ambayo aliwafanya wanaume kushindwa kuhimili kutofanya mapenzi naye ingawa hiyo imekuwa ngumu kwa Tim ambaye uamuzi wake na imani yake kama kijana aliyeokoka imepongezwa sana na hata watu kufikia kumpongeza kwamba anaishi kwa maneno yake kwakuwa vijana wengi waliokoka hushindwa katika kuhimili vishawishi vya uasherati.

Mmoja wa vijana aliyejikuta akibadilisha msimamo ni Nick Jonas ambaye alivyoanzisha uhusiano na msichana huyo alikaririwa akisema hawezi tena kusubiri kufanya mapenzi kabla ya ndoa kitendo ambacho yawezekana mrembo huyo alidhani angeweza kumwangusha kijana mwenye msimamo Tim Tebow ambaye amefanikiwa kuruka kiunzi. 

Tim Tebow ©epsnmediazone

Aidha kwa mujibu wa US Weekly umesema Tim alimuona Olivia kama mrembo haswa lakini urembo wake hauwezi kuvunja kiapo chake na Mungu, na katika kuonyesha hilo siku ambayo mrembo huyo alitangaza kuachana na Tim naye mwanamichezo huyo aliweka ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter akimshukuru Mungu kupitia neno la Zaburi 118 kama inavyosomeka chiniShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.