TAMASHA LA KRISMASI 2015 KATIKA PICHA

"Tarehe 25 Disemba, kila mwaka twakumbuka kuzaliwa mwokozi wa dunia, ndiye Yesu BWANA wetu. Sasa miaka mingi imekwishapita tangu mwana wa Mungu alipozaliwa, wengine imebaki historia tupu kwani bado hawajaokolewa."

Ndivyo kipande cha wimbo wa Naioth Prophetic Singers kilivyo, na hakika kwa mwaka 2016, kila mtu ameadhimisha sikukuu hii kinamna yake, wengine bar, wengine guest house, wengine kwenye nyumba za ibada, na wengine baada ya hapo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo Jijini Dar es Salaam, Gospel Kitaa ilikuwa sehemu ya kusanyiko lililofka kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa la Tanzania salama kwenye uchaguzi mkuu.

Waimbaji kadhaa wa kimataifa walikuwepo kukamilisha ratiba ya tukio hilo, wakiongozwa na Mwanamama Rebecca Malope kutoka Afrika Kusini. Tamasha hili limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotions.Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio siku hiyo, ambapo Kwaya ya Wakorintho wa Pili ilizindua album yake, mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, aliyewakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ndg Nape Nnauye.

Edson ZakoFaraja Ntaboba


Jessica BM

Sarah KChristina Shusho

Mlezi wa Chama cha Muziki wa injili Tanzania (CHAMUITA) Mbunge Martha Mlata akifurahia na kumtunza Christina Shusho.Bwana na Bibi Mlelwa
Martha Mwaipaja


Christopher Mwahangila


Solomon Mukubwa Mgeni rasmi akizindua album ya Kwaya ya Wakorintho wa PiliWaziri Nape Nnauye akisalimiana na wanakwaya wa Kwaya ya Wakorintho wa Pili punde baada ya kusindua album yao.
Mchungaji Emmanuel Mwasota akiomba

Askofu David Mwasota akiombea tukio
Mwenyekiti Mtendaji wa Msama Promotions, Alex Msama akihitimisha tukio la maombi.


Wakorintho wa Pili wakimtukuza Mungu jukwaani.

Faustin Munishi akimuelezea Malebo.Tutarejea na picha zaidi, endelea kufuatilia Gospel Kitaa.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.