TAMASHA LA KRISMASI NI KUBWA, HUSTAHILI KULIKOSA


Na Mwandishi Wetu

Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kimetoa wito kwa waamini kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CHAMUITA, Addo Novemba, tamasha hilo ni kubwa ambalo waamini hawastahili kulikosa kwa sababu ya umuhimu wa tamasha hilo.

Novemba alisema tamasha hilo lina dhamira mbili ambazo ni sikukuu ya kuzaliwa kwa Masiha na pili ni kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani, Oktoba 25 mwaka huu.

“Msama Promotions wanafanya kazi kubwa katika muziki wa injili na kumtangaza Mungu, hivyo ni nafasi ya waumini kujitokeza kumpa sapoti Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama ili kufanikisha matakwa ya jamii yenye uhitaji maalum,” alisema Novemba.

Naye Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentoste Tanzania, Askofu David Mwasota alisema tamasha hilo ni muhimu kwa sababu tumnasherehekea amani yetu.

Askofu Mwasota alisema wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya karibu kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo ni muhimu kwa Tanzania ijayo.

Askofu Mwasota alisema kusanyiko la wote ni kusanyiko la Mungu hivyo waumini wajitokeze kwa wingi ili kumrudishia Mungu shukrani baada ya kupita kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu.

“Tuanatam,bua kila mtu ana imani yake lakini tunatoa wito wa kila mmoija kukusanyika ili kumfikishia Mungu shukrani,” alisema.

Team GK itakuwepo, tukutane Diamond Jubilee leo mchana.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.