TAMASHA MIAKA 20 YA KANISA LA AIC DAYOSISI YA PWANI LAFANA JIJINI DAR ES SALAAMMwishoni mwa wiki iliyopita kulifanyika tamasha kubwa la uimbaji kuadhimisha miaka 20 tangu Kanisa la African Inland Church nchini (A.I.C (T)) Dayosisi ya Pwani kuanza huduma yake katika kanda hiyo. Tamasha hilo limefanyika katika ukumbi mkubwa wa PTA uliopo viwanja vya mwalimu JK Nyerere zamani Sabasaba vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Kwaya zinazolipa sifa kanisa hilo katika suala la uimbaji zilikuwepo ili kumrudishia Mungu utukufu kwa miaka hiyo ya huduma. Kati ya kwaya hizo ni pamoja na wana Ng'ang'ania baraka za Bwana AIC Shinyanga Choir, AIC Makongoro Vijana choir kutoka jijini Mwanza wakifahamika zaidi kwa jina la Kekundu, wengine ni pamoja na AIC Dar es salaam choir kutoka AIC Magomeni, AIC Chang'ombe choir (CVC) waite Gusa, Vunja au wana wa Tulia kwa Yesu bila kusahau AIC Neema Gospel Choir ambao wanatamba na album yao ya Haki yake Mungu. Pamoja na waimbaji wengine

Tamati ta maadhimisho hayo ambayo pia yalihudhuriwa na maaskofu wa dayosisi mbalimbali za kanisa hilo, yalihitimishwa na waziri mkuu mpya wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Majaliwa

Waziri mkuu Mh Majaliwa akiagana na maaskofu Silas Yego wa AIC Kenya, Askofu mkuu wa AICT S Kezakubi, Askofu John Bunango Dayosisi ya Mwanza, Askofu mstaafu Paul Nyagwasa (mfupi begani kulia kwa wazirimkuu) na Askofu John K Nkola wa Dayosis ya Shinyanga mara baada ya kuhitimisha sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya AIC Dayosisi ya Pwani 29/11/2015 katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam

Neema Gospel Choir (N.G.C)
AIC Makongoro Vijana Choir
AIC Dar es salaam Choir 
AIC Chang'ombe Choir (CVC)

Ukombozi Choir KKKT Msasani


AIC SHINYANGA


Picha ya pamoja baada ya kazi nzuri ya kumwinua Mungu, waimbaji wa CVC pamoja na madada kutoka AIC SHINYANGA.

Picha kwa msaada wa CVC, Lydia K, NGC

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.