WACHUNGAJI WAWILI NA WAKE ZAO NI MIONGONI MWA WALIOPOTEZA MAISHA AJALI YA SINGIDA


Ajali ya basi iliyotokea mkoani singida jumatatu usiku baada ya basi kugongana na Lori imefahamika kwamba ndani ya basi hilo walikuwemo wachungaji wawili na wake zao ambapo kwa pamoja walikua wakitoka jijini Dar es Salaam kwenye Kongamano la Wachungaji ambalo lilifanyika katika kanisa la Dar es Salaam Pentecostal Church.

Blog ya Mjap inc sambamba na kwenye ukurasa wa facebook wa kanisa hilo wameandika kama ifuatavyo na kuweka picha za wachungaji hao
DPC inasikitika kutangaza kifo cha wachungaji wawili waliopoteza maisha yao jana kwa ajali ya basi wakiwa safarini kuelekea Geita, Wachungaji hao ni kati ya wale waliotembelea kanisa la DPC na tuliabudu nao siku ya jumapili kuanzia ibada za asubuhi na Ibada ya kusifu na kuabudu. Askofu Lema Geita amefariki kwenye ajali hiyo. Habari kuhusu Mkewe bado tunaendelea kufuatilia, Tafadhali chukua wakati kuombea watoto wao waliowaacha na pia ombea makanisa waliokua wakiyaongoza, Mungu awe ndiye Nguzo ya kila kitu, Amina.
             BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.