BWANA HARUSI EDSON AKONGA MIOYO YA WADAU UZINDUZI WA DINA MGOMERA


Edson Zako Mwasabwite, kutoka ndani ya fungate moja kwa moja akatokea kwenye tamasha la uzinduzi wa albam ya Nina Haja Nawe, yake Dina Mgomera. Tukio la kupanda madhabahuni na kuimba wimbo wa kwa Neema tu, ambao ulitanguliwa na wimbo mwingine mpya, ulibariki umati wa watu, wasiochoka kumueleza Mungu kuwa yu mwema.

Kabla ya kuimba, alianza kwa kumshukuru Mungu kwa tukio la kupata mke, ambaye ni mwema, na kuwashukuru zaidi watu kwa kumpa sapoti kwenye tukio lake hilo la kiMungu. (bofya kuona picha za harusi)

Edson na Asley
Sanjari na hayo Edson aliomba wananchi kumsapoti kijana Asley, ambaye anachipukia kwenye tasnia ya muziki wa injili, huku akiwa na shauku ya kufanya kazi binafsi kama ailivyo kwa Edson.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.